29.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 4, 2023

Contact us: [email protected]

MATIC AWATISHA WAPINZANI

MANCHESTER, England

KIUNGO wa Manchester United, Nemanja Matic, amesisitiza kwamba wapo tayari kupambana na presha ya ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.

Kauli hiyo inatokana na mwanzo mzuri wa timu hiyo katika ligi hiyo.

Ushindi wa mabao  4-0 mfululizo katika michezo miwili ya West Ham na Swansea, inakifanya kikosi cha kocha wa timu hiyo, Jose Mourinho, kuongoza msimamo wa ligi hiyo baada ya kujizolea pointi sita na mabao nane.

Mourinho alikiri kwamba kikosi chake hakitapata ushindi kama huo kila siku hivyo wapo tayari kwa changamoto mpya itakayojitokeza.

Lakini Matic, ambaye alijiunga hivi karibuni akitokea Chelsea, anaamini kwamba United inaweza kupambana na presha ya ubingwa na kulitwaa taji hilo msimu huu.

“Unaweza kuwauliza wachezaji baada ya mchezo dhidi ya Swansea wanaweza kuwa na presha kutokana na mashabiki kutaka kuudhuria kila mchezo tutakaocheza kutokana na ubora wanaouona kwetu.

“Kila siku United kuna kitu kipya, kuna presha lakini kwa sasa tupo tayari kupambana nazo,” alisema Matic.

Matic alisema ana furaha kuwa United. “Wachezaji wote ni marafiki ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo, jambo ambalo ni muhimu.

“Msimu ni mrefu lakini kwa sasa tuna kikosi kizuri na mawasiliano mazuri pia, nafurahi kuwa miongoni mwao, huu ni mwanzo tu,” alisema Matic.

Nyota huyo aliongeza kwamba ni jambo la muhimu kujiamini kabla ya kufikiri kufunga bao uwanjani kwani kufanya hivyo kunaweza kukusaidia kuwa makini katika kila mpira.

“Kama unalinda vizuri unaposhambuliwa ni jambo zuri katika dakika 90 za mchezo, nina furaha kuwa miongoni mwa walinzi wanne wa United,” alisema Matic.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles