SHAHIDI: NILIKUTA KIPISI CHA SIGARA NYUMBANI KWA WEMA

0
874

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Mjumbe wa Shina Namba 39, nyumbani anakoishi Msanii wa Filamu, Wema Sepetu, Steven Alphonce amedai kilichokutwa nyumbani kwa msanii huyo ni kipisi cha sigara si bangi.

Mjumbe huyo amedai hayo leo Jumatatu Machi 12, katika Mahakama ya Halimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba akiongozwa na Wakili wa Serikali Constantine Kakula, wakati akitoa ushahidi wake katika kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili Wema na wenzake wawili.

Shahidi huyo amedai alishiriki upekuzi nyumbani kwa Wema na kukuta kipisi hicho cha sigara jikoni na chumbani kwa wema anakohifadhi viatu na nguo.

Amedia kuwa bangi anaijua ikiwa shambani kwani aliwahi kuiona Shinyanga lakini ikiwa nje ya hapo hawezi kuitambua.

Wema na wenzake wawili wanashtakiwa kwa kutumia dawa za kulevya aina ya bangi na walikamatwa Februari 4, mwaka jana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here