23.6 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yatakiwa kuwakamata wafanyabiashara meno ya tembo

ivory+pxHERIETH FAUSTINE NA IDDY ABDALLAH (RCT), DAR ES SALAAM

SERIKALI ya awamu ya tano imetakiwa kuwakamata na kuwashtaki wafanyabiashara wanaojihusisha na  biashara ya meno ya tembo.

Imetakiwa ichukue hatua hiyo bila kujali utaifa, hadhi na mamlaka waliyonayo watu hao.

Mjumbe wa Kampeni ya Okoa Tembo wa Tanzania, Lameck Mkuburo, alisema kufanya hivyo kutasaidia kuvunja mtandao wa ujangili   nchini.

Alikuwa akizungumza  Dar es Salaam jana alipotoa wito kwa serikali jinsi ya kukabiliana na tatizo la ujangili.

Mkuruburo alisema  miaka 50 iliyopita walikuwapo tembo  wapatao 300,000 nchini na mwaka 2014 walikuwa 109,000.

Alisema hivi  wamebaki 43,000 ambao ni asilimia 60 ya tembo waliokuwapo miaka mitano iliyopita.

“Tunaomboleza kwa upotevu wa maelfu ya tembo ambao walikuwa sehemu muhimu ya historia na alama ya taifa  letu,”alisema Mkuburo.

Alisema tembo  ni miongoni mwa vyanzo vikubwa vya pato la taifa katika sekta ya utalii ambako zaidi ya  watu milioni moja hutembelea hifadhi za taifa kila mwaka.

Watu hao huchangia asilimia 17 ya uchumi wa pato la taifa, alisema.

Alisema  juhudi zilizofanywa na serikali  katika  kukabiliana na tatizo la ujangili zinatambulika ikiwamo kuundwa mikakati ya  taifa dhidi ya ujangili.

Hata hivyo,  aliitaka Serikali kushughulikia chanzo kikubwa cha ujangili ambacho ni biashara ya meno ya tembo.

Alisema   urafiki wa  historia uliopo kati ya   Tanzania   na China unaweza kutumiwa  kufunga masoko ya meno ya tembo katika nchi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles