26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Walioua polisi Stakishari wasomewa mashtaka upya

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

UPANDE wa Jamhuri umewasomea upya mashtaka watuhumiwa 10 wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya watu saba wakiwamo askari.

Watu hao walifanya mauaji hayo kwenye    Kituo cha Polisi Stakishari wilayani Ilala, Dar es Salaam.

Mashtaka hayo yalisomwa upya jana  jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi, Thomas Simba.

Walisomewa mashtaka hayo muda mfupi baada ya kufutiwa kesi.

Kesi ilifutwa  baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Hellen Moshi  kuwasilisha hati ya  Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Kufutwa kwa kesi hizo kunatokana na upande wa Jamhuri kutaka kuunganisha  washtakiwa hao  kuwa katika hati moja ya mashitaka.

Washtakiwa hao ni  Omari Makota (28) mkazi wa Mbagala, Rajabu Ulatule (22)  wa Mkuranga na  Fadhil Lukwembe (23) kutoka  Chanika.

Wengine ni  Ally Mohamed maarufu kwa jina la Salum uso wa Simba Ulatule (63) mkazi wa Mkuranga, Hamis Mohamed au Salum Uso wa Simba Ulatule (57)  wa Mkuranga na Nassoro Abdallah (42), Uso wa Simba Ulatule.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles