23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yataja mikoa vinara uvutaji bangi

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

SERIKALI imesema matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi bado ni tatizo nchini, huku yakishika kasi katika mikoa ya Mara, Tanga, Morogoro, Arusha, Kagera na Ruvuma.

Wabunge Jumanne Kishimba (Kahama), Joseph Msukuma (Geita Vijijini), Ali Keisy (Nkasi Kaskazini) na aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari kwa nyakati tofauti waliwahi kutoa mapendekezo ya bangi kuhalalishwa.

Jana Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, akitoa taarifa ya hali ya dawa za kulevya kwa mwaka jana, alisema katika kipindi hicho vyombo vya dola kwa kushirikiana na wananchi walikamata tani 24.3 za bangi na watuhumiwa 10,061.

“Dawa za kulevya aina ya mirungi nayo imeendelea kutumiwa na watu wa rika mbalimbali hapa nchini, kwamba kwa mwaka 2018 vyombo vya dola vilifanikiwa kukamata tani 8.97 za mirungi zikiwahusisha watuhumiwa 1,186,” alisema.

Alisema katika kipindi cha mwaka jana, kesi 7,592 zikiwa na watuhumiwa 10,979 zilifunguliwa katika mahakama mbalimbali nchini, huku kesi 7,174 zilizowahusisha watuhumiwa 11,045 ziliendelea kusikilizwa.

“Serikali imeendelea kutoa huduma za tiba kwa watumiaji wa dawa za kulevya. Jumla ya vituo sita vilivyopo katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya na Dodoma viliendelea kutoa huduma, hadi mwaka 2018 zaidi ya watumiaji 8,000 waliendelea kupatiwa huduma za methadone katika vituo husika,” alisema.

Jenista alisema mwaka jana dawa za kulevya aina ya cocaine kilo 8.9 zilikamatwa, na watuhumiwa 156 walifikishwa katika mikono ya sheria.

Alisema kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC), Tanzania ilipunguza uingizaji wa dawa za kulevya nchini aina ya heroine kwa asilimia 90.

Kwa upande wake, Kamishna wa Kinga na Tiba kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Dk. Peter Mfisi, alisema Serikali hainunui dawa za methadone, bali zinanunuliwa na wafadhili kutoka Canada na thamani yake ni Dola za Marekani 1,500 kwa kilo moja.

Alisema nchini India kilo moja ya methadone ni Dola za Marekani 650 hadi 700, na kwa mwaka matumizi ya dawa hiyo hapa nchini ni kilo 300.

Dk. Mfisi alisema kilo moja ya methadone inahudumia watu 600 hadi 700 kwa mwezi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles