33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Maambukizi mapya ya Ukimwi Tanga yashuka

Na Amina Omari-TANGA

KASI ya maambukizi mapya ya ugonjwa wa Ukimwi katika Jiji la Tanga yameshuka kutoka asilimia tano mwaka juzi hadi asilimia 2.2 Julai mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Mratibu wa Ukimwi wa Jiji la Tanga, Mosses Kisibo wakati akiongea na gazeti hili kuhusu mikakati ya utekelezaji wa shughuli za ugonjwa huo kipindi cha mwaka huu.

Kisibo alisema kupungua huko kunatokana na hamasa ya elimu ya upimaji wa hiari waliyoitoa kwa jamii kuanzia ngazi ya shule za msingi.

“Kutokana na elimu ya upimaji wa hiari kuwafikia wananchi wengi, sasa kasi ya watu kujitokeza kupima imeongezeka kutoka watu 51,344 mwaka 2017 hadi kufikia watu 66,308 mwaka 2018,” alisema Kisibo.

Hata hivyo ili kuwalinda vijana na tabia hatarishi zinazosababisha maambukizi, Kisibo alisema wameshaanza kupeleka elimu ya mafunzo ya mifumo ya ustawi wa jamii na maswala ya Ukimwi kwa shule za msingi 15 na za sekondari 12 ndani ya jiji hilo.

Alisema miongoni mwa vyanzo vya ueneaji wa ugonjwa huo ni vitendo vya ukatili wa kingono, hivyo iwapo elimu itawafikia wanafunzi hao wataweza kujikinga dhidi ya vitendo hivyo na maambukizi.

Vile vile akiongelea uanzishaji wa dawa za kufubaza virusi vya ugonjwa huo, alisema kuwa wamefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 91 kuwaingiza katika matumizi ya dawa za ARVS waathirika hao.

Kwa upande wake, mratibu wa mradi wa afya kamilifu unaotekelezwa na Shirika la Amref, Dk. Edward Kilimba, alisema kuwa wamefanikiwa kupeleka bajeti ya Sh mil 158 kwa Halmashauri ya Jiji la Tanga ili kutekeleza miradi ya Ukimwi maeneo kinga, tiba na kuboresha mifumo ya utoaji takwimu.

“Tunaamini iwapo tutaweza kuwajengea uwezo wataalamu wa afya katika eneo la takwimu, wataweza kujua kwa haraka kama mikakati ya kupambana na ugonjwa huo inafanikiwa au laa,” alisema Dk. Kilimba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles