24 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yashauri wamiliki shule binafsi kuhusu ada

Ramadhani Hassan -Dodoma

SERIKALI imewataka wamiliki wa shule wote kutumia busara kutowarudisha wanafunzi nyumbani pindi shule zitakapofunguliwa kwa wazazi wao kutokuwa na ada.

Ushauri huo ulitolewa jana jijini Dodoma na Waziri wa  Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako wakati akizungumza na waandishi wa habari kutangaza ratiba za mitihani ya kitaifa.

“Wito kwa wamiliki wa shule kutumia busara kudai ada, shule zimefunguliwa ghafla, naamini baadhi ya wazazi walikuwa hawajipanga.

“Tuwe na moyo wa kupendana, wale ambao hawana ada tuweke ubinadamu ila na wale ambao hawajalipa kipindi ambacho kulikuwa kuna ugonjwa wa corona walipe.

“Sio vizuri kumkatalia mtoto wa masikini asiendelee na masomo, naamini kamati za shule zitakaa na kuweka utaratibu sawa,” alisema Profesa Ndalichako.

RATIBA YA MITIHANI

Katika hatua nyingine, Profesa Ndalichako alitangaza rasmi tarehe za mitihani ya taifa kwa watahiniwa  wa mwaka huu na mihula ya masomo kwa shule zote nchini.

Profesa Ndalichako alisema baada ya tangazo la Rais Dk. John Magufuli juzi wakati akivunja Bunge kuagiza masomo kuanza Juni 29, wizara yake imelipokea.

Alisema ratiba za mitihani kwa darasa la saba (PSLE) itafanyika kuanzia Oktoba 7 hadi 8.

Profesa Ndalichako alisema kidato cha pili (FTNA), itakuwa  kuanzia Novemba 9 hadi20, kidato cha nne (CSEE) kuanzia Novemba 23 hadi Desemba 11 na darasa la nne (SFNA) kuanzia Novemba 25 na 26.

Alisema  kwa shule za msingi na sekondari, wanafunzi watarejea shuleni Juni 29 na kumaliza muhula wa kwanza wa masomo Agosti  28, na kuanza muhula wa pili ambao utaisha Desemba 18.

Profesa Ndalichako alisema kwa wanafunzi wa kidato cha tano nao wataripoti shuleni Juni 29 kama ilivyotangazwa, na watasoma na kukamilisha muhtasari wa kidato cha tano na mitihani iifikapo Julai  24.

Alisema wataanza rasmi masomo ya kidato cha sita Julai 27.

“Niwasihi na kuwaomba wanafunzi wote kusoma kwa bidii, hatutakuwa na likizo, itakuwa ni kusoma tu labda mwezi wa nane watapumzika kidogo, lakini wataendelea na masomo kwa sababu wamepumzika muda mrefu kutokana na janga la ugonjwa wa corona,” alisema Profesa Ndalichako.

Alisema wizara inasisitiza uongozi wa shule zote nchini kuhakikisha wanafunzi, walimu na wafanyakazi wasio walimu wanazingatia maelekezo ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya ya ugonjwa wa corona.

 “Ninaomba niwatoe shaka, hakuna mwanafunzi yeyote aliyeugua corona mara baada ya kuwaruhusu kurudi shule,” alisema Profesa Ndalichako.

Alisema ili kukamilisha muhtasari wa masomo, shule zitalazimika kuongeza saa mbili za masomo kwa siku ili kufidia muda uliopotea..

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Tulichagua soko huriya na kuachana na Ujamaa, sasa haya ndio matokeo yake. Tulisema zamani Ubepari ni Unyama wengine wakacheka

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles