30.8 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaridhia mkataba wa Takwimu wa Afrika kwa masharti

Mwandishi Wetu, Dodoma


Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, amesema pamoja na Serikali kuridhia mkataba wa Takwimu wa Afrika, Serikali itawasilisha maombi maalumu ili kuiwezesha Tanzania kutotoa taarifa za takwimu ambazo nchi itaona zina usiri na utolewaji wake unaweza kuathiri maslahi ya taifa.

Dk. Mpango amesema hayo bungeni jijini Dodoma leo wakati akisoma mkataba wa azimio hilo.

Amesema utaratibu huo unatambuliwa kimataifa kupitia kupitia sehemu ya pili ya itifaki ya Vienna uliosainiwa mwaka 1969 ambapo Tanzania ni mojawapo ya nchi zilizoridhia kutumia mkataba huu tangu Aprili 12, mwaka 1976.

Dk Mpango amesema msingi wa azimio hilo ni mkataba wa kuanzisha Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika wa mwaka 1991 ambao Tanzania iliuridhia Januari 10, 1992 na Sheria ya Kuanzisha Umoja wa Afrika ya mwaka 2000 ambayo Tanzania iliridhia Aprili 6, 2001.

“Lengo kuu nyaraka hizi mbili ni kuhamasisha maendeleo ya kiuchumi maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa nchi Afrika na utangamano wa kiuchumi,” amesema.

Dk. Mpango amesema ili kutimiza lengo hilo nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU), waliazimia kuwa na mfumo wa pamoja wa kusimamia uzalishaji na usambazaji wa takwimu ili kuwezesha watunga sera na wataalamu wa mipango kuwa na uelewa mpana wa viashiria vya uchumi.

“Februari 4, 2009, wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika walilazimika kuwa na mkataba wa takwim Afrika kwa lengo la kuweka mfumo mfumo wa kuratibu upatikanaji na usambazaji wa takwimu bora za kiuchimi, kijamii na mazingira zitakazotumika katika kupanga na kutolea maamuzi maamuzi ya kisera katika ngazi ya kitaifa, kanda na bara la Afrika,” amesema Dk. Mpango.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles