24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Array

Kamati ya bajeti yataka usiri kwenye takwimu

Mwandishi Wetu, Dodoma



Kamati ya Bunge ya Bajeti, imeishauri Serikali kuhakikisha mamlaka za takwimu, watakwimu na wote wanaojihusisha na taasisi ya tasnia ya takwimu wanapaswa kuhakikisha uwepo wa ulinzi wa maisha binafsi, siri za kibiashara za watoa taarifa kama taasisi binafsi na za umma.

Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mashimba Ndaki, wakati akisoma maoni ya kamati yake kuhusu azimio la Bunge la kuridhia Mkataba wa Takwimu Afrika.

“Usiri wa taarifa zilizotolewa na taarifa hizo zitumike kwa malengo ya takwimu tu, aidha taarifa zinazomhusu mtu au taasisi zilizokusanywa kwa ajili ya takwimu kwa namna yoyote ile zisitumike katika mwenendo wa mahakama, hatua za adhabu au kufanya maamuzi ya kiutawala dhidi ya mtoa taarifa,” amesema.

Kamati hiyo pia ilishauri mkataba huo uifadhiwe pia kwa lugha ya Kiswahili tofauti na Serikali inavyosema kuwa utaifadhiwa kwa Kiarabu, Kiingereza, Kireno na Kifaransa.

 

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles