25.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaja na falsafa mbili kuimarisha Uhifadhi nchini

Na Faraja Masinde, Bagamoyo

Katika kuhakikisha kuwa sekta ya Utalii inakua na kuongeza mchango katika pato la Taifa Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imetangaza kuanza kutekeleza falsafa mbili ambazo ni Uhifadhi na Utangazaji utalii nchini lengo likiwa ni kuchochea ajira nchini.

Hayo yamebainishwa leo Februari 22, 2024 mjini Bagamoyo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara ya Maliasili na Utalii, John Mapepele aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, wakati akifungua Warsha ya siku mbili iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania(JET) kwa ufadhili wa  Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) kwa niaba ya Serikali ya Ujerumani (BMZ).

Warsha hiyo ambayo imelenga kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari za Mazingira 25 kutoka sehemu mbalimbali nchini ni sehemu ya Mradi wa Kupunguza Migongano ya Binadamu na Wanyamapori Tanzania utakaotekelezwa katika Ukanda wa Ruvuma.

Sehemu ya Washiriki.

Amesema kwa sasa wizara ina falsafa mbili kubwa za Uhifadhi  na Utangazaji utalii na hivyo mafunzo hayo lengo lake kuu ni kusaidia katika kuimarisha uhifadhi ili usaidie katika utangazaji Utalii suala ambalo ni muhimu kwa Taifa.

“Sekta ya Utalii inachangia asilimia 25 ya fedha za kigeni huku pia ikitoa asilimia 21 ya pato la Taifa na hivyo inapaswa kuangaliwa kwa umakini ikiwamo kuwekewa mikakati. Uhifadhi ukiimarika mazao ya uhifadhi pia yataimarika kama vile utalii na hivyo kulifanya Taifa kupata fedha za kigeni na kuimarisha uchumi wake kupitia hifadhi zetu

“Kwasasa Wizara imewekeza nguvu kubwa katika njia bora na za kisasa kutangaza Utalii na kuhifadhi na katika hili tunampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuimarisha uhifadhi ambapo amehakikisha uhifadhi unaendelezwa kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadae,” amesema Mapepele.

Mapepele pia amewahimiza  waandishi wa haabri waliopata fursa ya kushiriki mafunzo hayo kuyatumia kujenga uwezo kwa ajili ya kutoa habari za rasilimali kwa faida ya Taifa.

“Kwa siku mbili hizi za mafunzo,  tutumie fursa hii adhimu vizuri kwani itatusaidia sana kutujengea uwezo. katika nchi nyingi ambazo zimeendele hufanya haya tunayofanya leo,’’ alisema Mapepele.

Mkurugenzi Mtendaji wa JET, John Chikomo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET), John Chikomo ameishukuru GIZ na Serikali ambapo amebainisha kuwa mafunzo yatawasaidia waandishi kutoa Habari za migongano baina ya binadamu na wanyamapori kwa ufasaha na weledi mkubwa.

Mshauri wa mradi huo kutoka GIZ, Anna Kimambo.

Awali, Mshauri wa mradi huo kutoka GIZ, Anna Kimambo alisema kuwa mradi huo unatarajiwa kuwa na matokeo chanya kutoka maeneo ya mradi ikiwemo Liwale Mkoa wa Lindi, Namtumbo na Tunduru kutoka mkoa wa Ruvuma ambapo Vijiji 30, vitafikiwa katika mradi huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles