25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

SERIKALI YAITAKA TFF KUWALIPA WAAMUZI

WinfridA Mtoi-Dar es Salaam

BARAZA la Michezo la Taifa (BMT), limelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kulipa madeni wanayodaiwa na waamuzi na kuwachukulia hatua wale wanaoboronga.

BMT wametoa agizo hilo baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe, kuwataka kuchukua hatua kutokana na malalamiko ya waamuzi katika soka.

Mwakyembe alitoa agizo hilo, Februari 6, mwaka huu baada ya tuhuma nyingi zinazoelekezwa kwa waamuzi na TFF.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa BMT jana, Kaibu Katibu Mkuu wa baraza hilo, Neema  Msitha, alisema baada ya agizo hilo la Waziri Mwakyembe, walikutana na viongozi wa TFF na Bodi ya Ligi ili kubaini tatizo.

Alisema baada ya vikao hivyo na majadiliano ya kina, wametoa maelekezo mbalimbali kwa TFF, ikiwamo kuchukuliwa hatua waamuzi na maofisa wote wanaosimamia uendeshaji wa ligi bila kufuata sheria.

Alisema licha ya TFF kuanza kuchukua hatua, wanataka iwe endelevu kuhakikisha tatizo hilo linakwisha.

Agizo lingine ni kuboresha maslahi ya waamuzi na kuwalipa kwa wakati kwani TFF ilikiri kuwapo na changamoto ya malipo kutokana na kukosekana mdhamini katika msimu wa 2018/19.

“Tumejadiliana na viongozi wa TFF na Bodi ya Ligi, kuhusu waamuzi tumewashauri TFF wawalipe madai yao yoye, kama fungu halitoshi watafute vyanzo vingine vya fedha,” alisema Neema.

Alifafanua kuwa sababu iliyotolewa na TFF kushindwa kulipa waamuzi mapema ni kwamba fungu lililotengwa ni sh milioni 400, lakini mahitaji yakiwa ni takribani sh milioni 700.

Pia, BMT imelitaka shirikisho hilo kuwa na utaratibu wa kuandaa mafunzo ya waamuzi mara kwa mara ili kuwaongezea weledi kutokana na mabadiliko ya sheria.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,522FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles