26.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Serikali yaajiri watumishi wa afya wapya 307

Ramadhan Hassan -Dodoma

SERIKALI kwa kushirikiana na Taasisi ya Benjamin Mkapa imemwaga ajira 307 kada ya afya katika halmashauri 68 kuimarisha huduma za Ukimwi, kifua kikuu, malaria na magonjwa ya milipuko kama corona.

Pia Serikali ipo hatua za mwisho kukamilisha ajira za wataalamu wengine wa afya 80 watakaopangiwa kufanya kazi katika hospitali za rufaa za mikoa ya Shinyanga, Mara, Geita, Simiyu, Kagera, Kigoma, Tabora, Dodoma, Katavi na Mwanza.

Hayo yalielezwa jana jijini hapa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari akiongozana na Naibu wake, Dk. Faustine Ndugulile na Katibu Mkuu, Dk. Zainabu Chaula.

Ummy alisema taratibu za ajira kwa wataalamu wa afya 307 zimekamilika ambapo lengo kuu ni kuongeza nguvu katika sekta ya afya ili kuimarisha jitihada za kupambana na magonjwa ya Ukimwi, kifua kikuu, malaria pamoja na magonjwa ya milipuko kama Covid-19.

Alisema wataalamu hao wamepangiwa kufanya kazi katika mamlaka za Serikali za mitaa 68 zilizopo mikoa 11 nchini.

Ummy alisema kupitia mchakato huo wa ajira, kada sita za wataalamu wa afya zimenufaika na kibali hicho ambazo ni kada ya wauguzi wenye cheti 59, wauguzi wenye Diploma 30, maofisa tabibu 73, maofisa tabibu wasaidizi 100, wataalamu wa maabara ngazi ya cheti 25 na ngazi ya diploma 20.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,608FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles