28.4 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Nyongeza ya mishahara, kikokotoo cha mafao ajenda kuu ya TUCTA Mei Mosi

Sabina Wandiba -Dar es Salaam

NAIBU katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA), amesema wameazimia kuwasilisha kilio chao kwa Rais John Magufuli kuhusiana na ulipwaji mafao kwa viwango tofauti hali inayochangia kuleta migongano na manung’uniko kwa wafanyakazi.

Akizungumza na Mtanzania alisema jambo hilo ndiyo kipaumbele chao katika Sikukuu ya Wafanyakazi (Mei Mosi) mwaka huu ambazo kitaifa zinatarajiwa kufanyika Dodoma ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Magufuli.

Alisema, wafanyakazi wanakabiliwa na changamoto nyingi lakini katika maadhimisho ya mwaka huu 2020, wanatarajia kuwa na maazimio makubwa matatu iliwemo nyongeza ya mishahara, kodi na ulipaji mafao kwa wafanyakazi.

Akifafanua kuhusu maazimio hayo, Wamba alisema pamoja na Rais kutoa maagizo ya ya kufanyia ufumbuzi wa haraka suala hilo na kuwataka kuwa wavumilivu, bado inaonekana kuna tatizo katika utekelezaji wa agizo hilo.

“Bado tunaona lipo tatizo upande wa ulipaji mafao inayotokana na mifuko ya hifadhi ya jamii kwa wafanyakazi, wanalipwa kwa viwango tofauti na Rais Magufuli alishatoa agizo na zilishaundwa kamati mbali mbali na sisi tumeshirikishwa katika kamati hizo kusimamia suala hili lakini inaonekana bado kuna tatizo katika kupatiwa ufumbuzi,” alisema.

Alisema tatizo hilo linaleta mgawanyiko kwa wafanyakazi kwa kulipwa mafao kwa viwango tofauti na jambo hilo limetokea baada ya kufanyiwa marekebisho ya mfumo wa vikokotowa.

Alisema awali mfumo ulikuwa mmoja na sasa imebadilishwa na kuwa miwili ambapo mmoja ni ule wa wafanyakazi wanaolipwa asilimia 50, wengine wanapata asilimia 25 na wengine asilimia 75.

Akizungumzia kilio cha wafanyakazi katika ulipaji wa kodi, alisema bado wanalia kwa kutozwa kodi kubwa, hivyo wanaomba wapewe unafuu katika kodi ili kipato cha mfanyakazi kinapoongezeka kiwe na unafuu kidogo kwenye maisha yao kutoka na gharama za maisha kupanda.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles