23.2 C
Dar es Salaam
Monday, February 6, 2023

Contact us: [email protected]

SERIKALI YA RAIS ZUMA YAZIDI KUBANWA

PRETORIA, AFRIKA KUSINI

MAMIA ya raia wa Afrika Kusini wameandamana kwenye barabara za jiji la Pretoria kwa hofu kuwa huenda wizara ya ustawi wa jamii nchini humo ikashindwa kufanya malipo ya mafao kwa mamilioni ya watu masikini nchini humo.

Maandamano hayo yameongozwa na kinara wa upinzani kutoka chama cha DA, Mmusi Maimane, yaliyokuwa baada ya majuma kadhaa ya hofu ya kushindwa kuhudumiwa kwa watu masikini zaidi ya milioni 17.

Inahofiwa kuwa huenda malipo hayo yasifanyike kabisa baada ya Serikali kushindwa kutangaza kampuni mpya iliyopewa jukumu la kusimamia na kugawa fedha hizo kwa watu masikini huku mkataba wa mtoaji wa sasa ukifikia mwisho Machi 31, mwaka huu.

“Chini ya wiki tatu zijazo, mamilioni ya raia wa Afrika Kusini wanaelekea kukosa mafao yao ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa kulipa fedha hizo. Robo tatu ya raia wetu wanategemea msaada huu kutoka serikalini kuishi,” amesema Maimane.

Maandamano haya yalihitimishwa nje ya ofisi za waziri wa masuala ya ustawi wa jamii, wengi wakiwa na mabango ya chama cha upinzani cha Democratic Alliance. Kiasi cha randi milioni 140 sawa na dola za Marekani bilioni 10 hutolewa kila mwaka kwa watu masikini.

Chama tawala nchini Afrika Kusini, ANC, ambacho kinapambana kutopoteza umaarufu, kimekuwa kikitumia malipo haya kuwalipa wazee, watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu ili kujenga imani toka kwa watu masikini.

Mfumo wa ulipaji wa mafao kwa watu masikini nchini Afrika Kusini ulianza kuingia dosari mwaka 2014 wakati mahakama kuu ilipotoa uamuzi kuwa kampuni ya sasa ilipewa zabuni hiyo kinyume cha sheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles