22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali ya Kenya yamkana Jaguar, Bunge kumchukulia hatua

Anna Potinus

Serikali ya Kenya imekanusha kuhusika na kauli aliyoitoa Mbunge wa Starehe nchini humo, Charles Njagua maarufu Jaguar, aliyewatuhumu raia wa kigeni wakiwamo Watanzania kuchukua biashara za Wakenya na hivyo kuwataka waondoke ndani ya saa 24.

Katika video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii jana, Mbunge akiwahutubia wananchi nchini humo pia alitoa saa 24 kwa Serikali ya Kenya kuwaondoa raia hao na wasipoondoka  watawapiga na kuwaamuru kuondoka kwa nguvu kauli iliyoshangiliwa na wananchi wakionyesha kuunga mkono suala hilo.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa na Msemaji wa Serikali, Cyrus Oguna, imesema serikali ya nchi hiyo haihusiki kwa namna yoyote na kauli aliyoitoa Mbunge huyo na kwamba kauli hiyo haina nafasi kati mazingira ya dunia ya sasa.

“Wakenya ni watu wenye upendo na amani na kwa miaka mingi tumekuwa tukiishi na raia wa mataifa mbalimbali bila tatizo lolote. Hii ni thamani ambayo tunajivunia kama taifa na ni lazima tuendelea nayo.

“Tungependa kusema kuwa huo si msimamo wa Serikali ya Kenya na tunashutumu matamshi hayo yaliotolewa katika video inayosambaa katika mitandao na bunge linachukulia yaliyomo katika hiyo video kwa uzito mkubwa na tayari imeanza kuchukua hatua kali za kisheria,” imesema taarifa hiyo.

Hata hivyo, baada ya kauli hiyo ya Jaguar, jana Serikali ya Tanzania haikukaa kimya ambapo iliwataka raia wake kuwa watulivu huku Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisema Serikali imechukua hatua dhidi ya kauli hiyo ikiwa ni pamoja na kumwita Balozi wa Kenya nchini kufahamu msimamo wa kauli hiyo, ambaye ameeleza huo si msimamo wa nchi yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles