27.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 20, 2023

Contact us: [email protected]

Kalemani amshusha pumzi Kawambwa mradi wa REA jimboni kwake

Anna Potinus

Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani amemtoa hofu Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Shukuru Kawambwa, kuhusu kutekelezwa kwa mradi wa umeme katika Kijiji cha Kondo kilichopo katika Kata ya Zinga kilichokuwa kwenye mradi wa REA awamu ya pili, ambacho hadi Juni mwaka 2016 hakikutekelezewa mradi wake.

Dk. Kalemani ametoa kauli hiyo bungeni leo Jumatano Juni 26, alipokuwa akijibu swali ya nyongeza la mbunge huyo aliyetaka kupata kauli yake juu ya utekelezaji wa mradi huo.

Kawambwa amesema ndani ya kijiji hicho kuna Shule ya Msingi ya Kondo na Sekondari ya Zinga na miundombinu yote haina umeme hadi sasa.

Akijibu swali hilo, Dk. Kalemani, vijiji vyote vimeshapata umeme na hivi sasa vimebakia vitongoji tu.

“Kati ya Wilaya ambazo vijiji vyake vyote vimeshapata umeme ni pamoja na Bagamoyo.

“Kuna vitongoji 169 katika Jimbo la Mheshimiwa Mbunge na kati ya hivyo vitongoji 100 tayari vina umeme bado 69 tu ambavyo bado havijapata umeme ambavyo ni pamoja na kitongoji cha Kondo, kwa hiyo nimpe mheshimiwa Mbunge imani kwamba nimeshawaelekeza wakandarasi wakishirikiana na Tanesco wameshaanza kupeleka umeme kwenye kitongoji cha Kondo na watakamilisha Julai 12 hivyo asiwe na wasiwasi,” amesema.

Aidha, Dk. Kalemani ameongeza kuwa Mkandarasi aliyeko katika Jimbo la Bagamoyo na Chalinze anapeleka umeme katika vitongoji vyote ikiwemo kijiji kirefu cha Msingi na Magurumatare cha kilomita 28 ambacho hakijapelekewa umeme.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles