25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali ya ahidi kusaidia Vijana

Na Safina Sarwatt, Moshi

Naibu waziri  Ofisi ya waziri mkuu  anayeshugulikia kazi,vijana na ajira Patrobasi Katambi amesema serikali iko tayari kuwasaidia vijana ambao  wameonyesha uwezo wa kuanzisha viwanda vidogo vidogo na kuanza uzalishaji wa bidhaa mbalimbali, hatua ambayo itaisadia kukuza uchumi wa taifa na kuzalisha ajira.

Katambi ameyasema hayo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro wakati wa maonyesho ya shughuli mbalimbali za ujasirimali zinazofanywa na vikundi mbalimbali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha ushirika Moshi.

Amesema kuwa lengo la Serikali ni kuanzisha viwanda ili kuongeza ajira kwa vijana na kuongeza mapato na kwamba amefurahishwa na hatua za wanafunzi wa chuo kikuu cha ushirika Moshi kuanzisha vikundi mbalimbali za ujasirimali  ambazo zinajihusisha na uzalishaji  bidhaa mbalimbali.

Amesema serikali itahakikisha inaboresha mazingira ya ujasirimali kwa vijana wanaojihusisha na shughuli za uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ,ikiwa ni pamoja na kuwasaidia mikopo na kuwatengea maeneo maalumu ya kunzisha viwanda vidogo.

“serikali iko tayari kuwasaidia vijana wote  wanaojishughusha na shughuli za uzalishaji bidhaa mbalimbali kwa kuhakikisha bidhaa zote zinakuwa na ubora unaotakiwa katika soko la ndani na nje,”amesema.

Makamu mkuu wa chuo kikuu cha ushirika Moshi,prof Alfredy Sife amewataka vijana kutafuta fursa mbalimbali za kiuchumi na kujiajiri sambamba na kuwa nidhamu ya matumzi ya fedha.

Meneja wa mfuko wa jamii (NSSF)mkoa wa Kilimanjaro Large Materu amesema shirika hilo limejipanga kusaidia vijana na vikundi vya wajisiriamali vinavyojihusisha na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali,waliko katika mfumo usio rasmi,kwa kuwapatia mikopo kuanzia shilingi million moja hadi million 50.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles