24.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 30, 2023

Contact us: [email protected]

Profesa Mwansisya ataja visababishi vya Magonjwa ya akili

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

MATATIZO katika ndoa, ugumu wa maisha,u kosefu wa chakula,vimetajwa ni visababishi vya magonjwa ya akili wakati wa kipindi cha uzazi.

Hayo yameelezwa na Mhadhiri kutoka  Chuo Kikuu cha Agha Khan cha Jijini Dar es salaam, Profesa  Tumbwene Mwansisya wakati akizungumza katika  mafunzo  kwa wahudumu 29  wa sekta ya afya Jijini Dodoma  juu ya kumtambua mtu mwenye ugonjwa wa akili na jinsi ya kumtibu katika kipindi cha uzazi.

Profesa  Mwansisya amesema sababu ya ukubwa wa tatizo la ugonjwa wa akili katika kipindi cha uzazi ni mahusiano ambapo amedai ndoa nyingi zimekuwa na changamoto hali ambayo inafikia mama mjamzito kuwa na mawazo mengi hivyo kupata ugonjwa huo.

“Siku hizi kunachangamoto sana katika mahusiano watu wenye ndoa ndio wanauana sana,ugumu wa maisha,kukosa chakula hivyo kukosa matunzo na pia jamii inavyomchukulia mtu.Matatizo yanaweza yakawa kwa mtu ama mabadiliko ya homoni au changamoto za maisha,”amesema Prof.Mwansisya.

Prof.Mwansisya amesema  madhara yake ni kwa mama hawezi kuwa na mahusiano mazuri na mme wake na mtoto wake wa kumzaa ambapo pia amedai kutakuwa na shida katika jamii kwani baba anaweza  kuanzisha familia nyingine.

Amesema tiba yake ni dawa ,matibabu ya kisaikolojia kwa kupewa ushauri nasaha,matibabu ya kijamii na matibabu ya kiroho.

Akielezea mafunzo hayo amesema  yamelenga jinsi gani ya kutambua mtu mwenye ugonjwa wa akili jinsi ya  kumtibu na kuzuia mama ama baba anaenda Kliniki  kwa ajili ya uzazi na  jinsi gani aweze kutibiwa.

“Kwa kawaida kipindi cha uzazi huwa kinaambatana na magonjwa ya akili lakini kwa bahati mbaya sana kipindi hichi cha uzazi wengi hawajafundishwa jinsi ya kutambua magonjwa ya akili na jinsi ya kutibu ndio maana tukaja na mafunzo haya ili kuweza kuitatua hii changamoto,”amesema Profesa Mwansisya ambaye pia ni Daktari bingwa wa magonjwa ya akili,”amesema

Amesema wamekuwa wakifundisha  magonjwa gani ya akili ambayo yamekuwa yakitokea,jinsi ya kutambua kama  mama mjamzito ana ugonjwa huo pamoja na  jinsi ya kumtibu.

Prof. Mwansisya   amedai kwa pomoja  wamejadiliana mikakati ya kuangalia jinsi ya kutengeneza huduma kwenye kadi ya mama ili mama mjamzito   aweze kuulizwa maswali pindi anapofika Kliniki ili iwe rahisi kuweza kujua tatizo mapema.

Amesema tatizo hilo ni kubwa kwani utafiti mwingi umekuwa ukifanywa mjini bila kufika maeneo ya vijijini.

Kwa upande wake,Daktari wa Afya ya akili kutokea kituo cha  afya cha Makole,Zahati Shamahonge amesema mafunzo hayo yamemsaidia kupambanua, kujua mama anapokuwa mjamzito kuna mabadiliko ambayo yanatokea mwilini mwake hivyo anatakiwa kupewa huduma zipi ili kuweza kujua tatizo.

“Inapelekea yule mama kubadilika kitabia kimaono na vitendo mama mjamzito anapopata mimba jamii inatakiwa imsapoti kuanzia lishe na kila kitu,kuna wengine wanapata mimba za utotoni tusimshangae tukimshangaa anaanza kuhisi vibaya na anaanza kupata msongo wa mawazo,”amesema

Naye,Mratibu wa afya ya akili Wilaya ya Dodoma Mjini,Asnati Mgeni amesema mafunzo hayo yamemsaidia kujua jinsi gani ya kuwasaidia wenye matatizo pamoja na kujua ukubwa tatizo.

“Saa zingine watu walikuwa wanajua kwamba kalogwa au hachangamani kumbe ni shida ambayo anakuwa ameipata katika akili zake,”amesema.

Amesema katika Wilaya ya Dodoma tatizo hilo  ni kubwa kwani asilimia zaidi ya 80 wana tatizo hilo huku wengi wakiwa hawajui.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,203FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles