22.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Serikali: NMB kinara utatuzi wa changamoto za elimu, afya nchini

…Shule 8 Temeke, Ulanga zapewa misaada ya Sh mil 43.8/-

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Serikali imeitaja Benki ya NMB kama kinara wa usaidizi katika utatuzi wa changamoto kwenye Sekta za Elimu na Afya nchini, kauli inayokuja huku benki hiyo ikitoa misaada mbalimbali yenye thamani ya Sh milioni 43.8 kwa shule nane, tatu kati ya hizo kutoka Wilaya ya Temeke na tano za Wilaya ya Ulanga, Morogoro.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe (katikati )akimshukuru Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard baada ya kumkabidhi mabati 576 yenye thamani ya Sh milioni 18 yaliyotolewa na Benki ya kwa Shule za Msingi za Yombo Dovya, Tuangoma na Faraja wakati wa hafla iliyofanyia jana.Serikali imeitaja Benki ya NMB kama kinara wa usaidizi katika utatuzi wa changamoto kwenye Sekta za Elimu na Afya nchini.

Hayo yamesema na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe, wakati akipokea msaada wa mabati 576 yenye thamani ya Sh milioni 18, kutoka NMB kwenda kwa Shule za Msingi Yombo Dovya, Faraja na Toangoma zilizopo wilayani mwake, kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard. 

Akizungumza wakati wa kupokea msaada huo, kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Yombo Dovya, DC Gondwe amebainish libainisha kuwa, NMB imedumisha utamaduni chanya wa kujitoa, mara nyingine bila kuombwa, kutatua changamoto kusapoti sera ya Elimu Bure, ambako Serikali inatumia zaidi ya Sh bilioni 3.5 kwa kwa shule za wilaya yake tu.

Amebainisha kuwa, Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inatumia takribani Sh bilioni 1.8 kwa Shule za Sekondari na Sh bilioni 1.7 kwa Msingi kwa mwaka, ambazo zinaweza kuwa hazitoshi, lakini uungwaji mkono inaopata kutoka kwa wadau wa elimu hasa NMB, umefanikisha maboresho ya mazingira ya kufundisha kwa walimu na kujifunza kwa wanafunzi.

“Hii Programu ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), ya NMB ni nzuri na ni jambo kubwa mno mnafanya. Mmekuwa vinara wa kusapoti jitihada za Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, tena mara nyingine mmefanya hivyo bila kusubiri kuombwa kusaidia katika wilaya yetu na Tanzania kwa ujumla,” amesema Gondwe, aliyefichua kuwa ukongwe na uchakavu wa shule nyingi wilayani mwake, umeongeza uhitaji wa misaada.

Akaongeza kuwa, uthibitisho mwingine wa namna NMB inavyojitoa kustawisha Sekta za Elimu na Afya, ni uamuzi wa benki hiyo kuunda timu maalum iliyopita mashuleni, hospitalini, zahanati na vituo vya afya wilayani Temeke, kukagua maeneo yanayohitaji usaidizi, sambamba na kuona matumizi ya misaada iliyokwishatolewa.

Kwa upande wake, Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, alisema benki yake inaishukuru Serikali pamoja na viongozi na walimu wa shule mbalimbali wilayani Temeke na Tanzania kwa ujumla, kwa kuichagua NMB kuwa mshirika sahihi katika utatuzi wa changamoto za elimu.

Aliongeza kuwa, kupitia CSR, NMB inajisikia fahari kudumisha utaratibu endelevu wa kutumia asilimia 1 ya faida yake kila mwaka, kusaidia kwenye sekta za Elimu na Afya, pamoja na majanga kama mafuriko na kimbunga  yanapotokea, utamaduni ambao wamekuwa wakiufanya kwa miaka kadhaa sasa, lengo likiwa ni kuinga mkono serikali na kurejesha kwa jamii.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Yombo Dovya, Salum Gawaza, alisema shule yake iliyoanzishwa mwaka 1995, hivi sasa ikiwa na wanafunzi 2270 na walimu 48, imekuwa na changamoto nyingi zinazotokana na uchakavu wa vyumba vya madarasa, Ofisi na miundombinu, na kwamba msaada wa NMB unaenda kuzipunguza, huku akiwataka wadau zaidi wa elimu kufuata nyayo za benki hiyo.

Wakati huo huo, Benki ya NMB kupitia Meneja wa Kanda ya Mashariki, Dismas Prosper, imekabidhi misaada yenye thamani ya Sh milioni 25.8 kwa shule mbalimbali wilayani Ulanga mkoani Morogoro, yakiwemo mabati 234 na kofia zake 14, mbao 248, misumari kilo 100 na madawati 150.

Msaada huo, uliopokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Ngollo Malenya, kwa niaba ya uongozi wa Shule za Msingi Namgezi, Kwiro, Mbasa, Mahenge na sSekondari ya Lupilo, unaenda kumaliza adha ya wanafunzi kutoka Kijiji cha Namgezi kusafiri kilomita 8 kila siku ya masomo kwenda Shule ya Msingi Makanga walikokuwa wanasoma.

Kwa mujibu wa mgawanyo wa vifaa hivyo, Shule ya Msingi Namgezi, itapata mabati 108 na kofia zake 14, mbao 120 na misumari kilo 50 kwa ajili ya kupaulia vyumba vya madarasa vya shule hiyo mpya kabisa, ambayo itakuwa mkombozi wa watoto wa kijiji hicho, waliokuwa wakichelewa masomo kwa wastani wa masaa mawili kila siku.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,305FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles