22 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

Viongozi wa Uamsho waachiwa huru

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Viongozi wawili kati ya 36 wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI), Sheikh Farid Hadi Ahmed na Mselem Ali MselemĀ  waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya ugaidi wameachiwa huru.

Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Sylvester Mwakitalu amesema leo Jumatano Juni 16, 2021 kuwa amewafutia mashtaka viongozi wote wa jumuiya hiyo na kilichobaki sasa ni taratibu za kutoka gerezani.

Wawili hao ambao  walikuwa mahabusu tangu mwaka 2014 pamoja na wenzao kutokana na kukabiliwa na mashtaka hayo ambayo hayana dhamana wameachiwa huru jana Jumanne Juni 15, 2021  baada ya DPP kuwafutia mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili.

Aidha, taarifa za kuachiwa huru kwa viongozi hao zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuanzia jana jioni zikieleza kuwa viongozi hao wawili ndio wameachiwa huru na mmoja wa mawakili wao, Juma Nassoro amelieleza kuwa wameshapelekwa majumbani mwao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,284FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles