25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 1, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kuwezesha ujenzi wa vituo vya mafuta vijijini

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inatarajia kuanzisha mradi wa kujenga vituo vipya vidogo vya mafuta maeneo ya vijijini (petroli na dizeli) vya gharama nafuu ili kuondoa changamoto za usafirishaji zitokanazo na njia zisizo salama na wadau kuomba mikopo itatolewa na Serikali.

Hayo amezungumza Julai 3, jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa jukwaa la wadau wa Mafuta na Gesi Asilia, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Injinia Felchesm Mramba katika viwanja vya maonesho ya 47 maarufu Sabasaba yanayoendelea nchini ambapo amesema nishati ni muhimu kwa maendeleo ya uchumi.

Jukwaa hilo limeandaliwa kwa ushirikiano na Kampuni ya Madini TANZAKWANZA na Mamlaka ya Biashara Tanzania (Tantrade) lengo kubwa kukutanisha wadau kutoka serikalini na sekta binafsi kujadili changamoto mbalimbali.

“Mwisho kuwasilisha maombi ya mkopo wa mradi kujenga vituo vya mafuta vijijini ni Agosti 25, mwaka huu na wadau wa mafuta kuomba mkopo ambao serikali itatolewa kupitia REA ili kuwezesha ujenzi na uendeshaji wa vituo vipya vidogo vya gharama nafuu vijijini na kuwafikia huduma kwa urahisi,” amesema Injinia Mramba.

Amesema serikali kwa sasa ipo katika mchakato wa kuhakikisha kuwa inapeleka gesi kwenye nchi jirani kama Kenya, Uganda na Zambia, na inahimiza watanzania na wawekezaji kutoka nje kuja kushirikiana katika kuendeleza gesi asilia na isiwe katika kuchimba pekee.

Amesema asilimia 60 hadi 70 ya umeme unaozalishwa nchini unatokana na gesi asilia hivyo ni wakati Sasa kujiendeleza na kufikia nchi hizo. Tanzania imefungua mikono yake kwa Uwekezaji wenye tija.

Aidha, amesema hivi karibuni, serikali ilifanya maamuzi ya kuendeleza gesi hiyo kupitia mradi wa kuibadili kutoka katika hali hewa na kuwa katika hali ya kimiminika (LNG Project), ili iweze kusafirishwa kwa wingi kwenda kuuzwa katika masoko ya Kimataifa.

Amesema mradi huo mkubwa wenye thamani ya Sh trilioni 70 ni fursa kwa wawekezaji na wafanyabiashara kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika.

Amesema biashara ya mafuta imeathiriwa mno na vita vinavyoendelea kati ya Ukraine na Urusi vikwazo ilivyowekewa Urusi vimesababisha upatikanaji mdogo wa mafuta ulimwenguni.

“Hii ni kwa kuwa Urusi ni nchi ya tatu duniani kwa uzalishaji wa mafuta. Meli za mafuta kutoka Urusi zimezuiliwa kusafirisha mafuta hata kutoka nchi nyingine. Haya yote yamechangia kupanda kwa bei ya mafuta,” alisema na kuongeza kuwa serikali imechukua hatua kadhaa kuhakikisha kuwa nchi inakuwa na mafuta ya kutosha lakini pia gharama za bidhaa hii hazimuumizi mtanzania wa kawaida.

Amesema mkakati wa ruzuku ambao umewezesha bei ya mafuta, mfano dizeli kushuka kutoka Sh 3,454 mpaka kufikia Shilingi 2871 kwa sasa.

Amesema serikali inajitahidi kuweka mikakati madhubuti ya utekelezaji ambayo itawasaidia wafanyabishara wa mafuta kukabiliana na changamoto za kuadimika kwa mafuta ulimwenguni.

Amesema ushirikiano na ushiriki wa taasisi binafsi ni muhimu sana katika kufanikisha malengo ya kuongeza upatikanaji wa nishati ya mafuta na gesi asilia kwenye maeneo ya vijijini kama ilivyofanya katika kusambaza umeme kupitia REA.

Mramba amesema muda wowote kuanzia sasa mikataba ya kuweka gesi asilia kwa njia ya kimiminika itasainiwa na mradi huo utakuwa mkoani Lindi ambapo utabadilisha kwa kiwango kikubwa uchumi wa nchi,maisha ya watu na kuongeza kiwango cha gesi kutumika nchini na nje ya nchi.

Amesema kuputia jukwaa hilo serikali inatarajia majadiliano ya kina na yenye kuleta maendeleo katika sekta ya mafuta na gesi asilia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles