29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

TTCL yajivunia matunda ya ukuaji wa Teknolojia

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeendelea kujivunia matunda yatokanayo na ukuaji wa Teknolojia ambapo hivi sasa limekuwa likitangaza utalii kidigitali ikiwemo kupiga picha mubashara wakati wa kupanda Mlima Kilimanjaro.

Akizungumza Julai 3, jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari alipotembelea banda la TTCL lilipo kwenye maonyesho ya biashara ya 47, Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika hilo Zuhura Muro amesema ukuaji huo wa Teknolojia umechochea kukuza sekta ya utalii kwani unaweza kumshuhudia mtalii akiwa kwenye vivutio mbalimbali mubashara kwa kutumia mfumo wa kisasa iliyopo katika shirika.

Amesema shirika hilo linafungua nchi katika uchumi wa kidigital kwani sasa wanauwezo wa kuendesha vituo vya mawasiliano (call center) ambavyo vimefungwa kwenye taasisi mbalimbali kote nchini.

“Ukuaji huu wa Teknolojia kwetu sisi kama TTCL unatusaidia kuifungua nchi ukiacha kutangaza utalii kidigitali lakini pia tunaweza kuunganishi nchi lakini hata kuuza ubunifu wa teknolojia tulionao,” amesema Muro.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TTCL, Peter Ulanga amesema wamekuja na huduma kwa wananchi ya kuwafikishia huduma ya mtandao mpaka nyumbani.

“Sasa hivi tunahakikisha uchumi unakua kidigital ndio maana tumekuja na mpango wa kufikisha huduma ya mtandao mpaka nyumbani ifahamikayo kama, Fiber Mlangoni hii ni rahisi na itasidia kila mwananchi anatumia mtandao katika shughuli zake za kila siku,”amesema Ulanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles