23.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Singida Fountain Gate yalamba mamilioni Sportpesa

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

KAMPUNI ya Sportpesa imeikabidhi klabu ya Singida Fountain Gate kitita cha fecha Sh milioni 50 ikiwa ni bonasi ya kumaliza nafasi ya nne katika msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Julai 3, 2023 wakati akikabidhi mfano wa hundi kwa uongozi wa klabu hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Sportpesa Abbas Tarimba amesema fedha hizo ni motisha kutokana na kuridhishwa na juhudi iliyofanywa na timu hiyo.

“Tumetoa fedha hizi kama motisha kwa ajili ya kuridhishwa na juhudi iliyofanywa na timu hii msimu uliopita endapo wangemaliza wakiwa juu zaidi ya hapo tungewapa kubwa zaidi ya hii tuliyowapa leo, amesema Tarimba.

Amesema timu hiyo imepiga hatua kubwa katika Ligi Kuu jambo ambalo linazidi kuwapa matumaini ya kuendelea kufanya nao kazi.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Singida Fountain Gate,John Kadutu amejitapa kuwa fedha hizo zimewaongezea hamasa na kuwataka waliopo juu yao wajipange msimu ujao kutokana na aina ya usajili wanaokwenda kuufanya.

“Udhamini huu unazidi kutupa nguvu, tutahakikisha msimu ujao tunazishusha timu zilizopo juu kutokana na usajili tutakaoufanya. Nawaambia kabisa wajipange,” amesema Kadutu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles