20.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 28, 2022

SERIKALI KUTENGA FEDHA KUKUZA UBIA SEKTA ZA UMMA, BINAFSI

 

|Susan Uhinga, TangaSerikali imesema itaendelea kutenga fedha kwa ajili kuwajengea uwezo wataalamu wa wizara na halmashauri wanaotekeleza mpango wezeshi wa kukuza ubia wa sekta ya umma na sekta binafsi (PPP) ili waweze kusimamia na kutekeleza miradi ya maendeleo.

Akifungua mafunzo ya siku tano ya maofisa wa wizara na halmashauri kutoka wilaya 60 nchini, Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Injinia Zena Saidi, amesema licha ya serikali kuandaa muswada kwa ajili ya kusimamia mfumo wa PPP, lakini pia itaendelea kutoa fedha za mafunzo.

“Mafunzo mnayoyapata leo ni muendelezo wa mafunzo kama haya yaliyofanyika mwaka 2004 na wataalamu wapatao 500 walipatiwa mafunzo hivyo serikali itaendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuwapatia mafunzo ili mpango huo uweze kutekelezwa kwa mafanikio,” amesema Katibu Tawala huyo.

Aidha, amesema Juni 29 mwaka huu muswada wa sheria kwa mpango huo ulisomwa kwa mara ya kwanza bungeni na kwamba utapelekwa utapelekwa tena kabla haijawa sheria lengo ikiwa ni kusimamia mpango wezeshi kwa miradi ya PPP na wawe tayari kutoa maoni yao.

Katibu Tawala huyo amesema utaratibu wa mfumo huo ni utekelezaji unaotoa fursa nzuri kwa miradi inayotekelezwa kwa ushirikiano wa jamii na wabia ambapo nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara imeweza kutekeleza miradi ipatayo 383 yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 69.

Naye Kamishna wa PPP Wizara ya Fedha  na Mipango, Dk. John Mboya amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo watendaji wa halmashauri hizo na wale wa wizarani  kuendeleza miradi ya PPP na inayotekelezwa na Serikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,097FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles