24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

TCRA KUIFUNGIA STAR TIMES

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam


Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), inakusudia kusimamisha leseni zote zilizotolewa na mamlaka hiyo kwa Kampuni ya Star Media (Star Times Ltd), kwa kushindwa kutekeleza amri na masharti ya kuruhusu watazamaji wake kutazama chaneli ambazo zinatakiwa kuonyeshwa kupitia ving’amuzi vyao bila malipo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo leo Agosti 13, imesema imekusudia kuchukua hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko ya watazamaji ambapo Juni mwaka 2016, ilifanya uchunguzi juu ya malalamiko hayo na kubaini kuwa kampuni hiyo haitimizi wajibu wake kwa kuwa inawatoza watazamaji wake fedha kwa chaneli zinazotakiwa kutazamwa bila malipo.

“Hivyo basi, kwa kuwa kampuni hiyo ya Star Media Tanzania Limited, imevunja sheria na imekaidi kutekeleza amri halali ya TCRA kwa kukataa kulipa faini na kwa kuendelea kuwatoza watazamaji wa chaneli za televisheni ambazo zinatakiwa kutazamwa na wateja wake kupitia ving’amuzi vya Star Times bila malipo, kwa mamlaka iliyo nayo TCRA inautangazia umma kuwa inakusudia kusimamisha leseni zote zilizotolewa na TCRA kwa kampuni hiyo kwa kushindwa kutekeleza amri halali ya mamlaka hiyo,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Hivi karibuni, TCRA imeziamuru Kampuni za DSTV na Zuku, kuondoa chaneli zote za kitaifa zikiwamo ITV, Channel Ten, Clouds TV, Wasafi TV na nyinginezo na kubakisha Kituo kimoja pekee cha Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles