27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kushughulikia changamoto ya miradi kutokukamilika kwa wakati

Na Malima Lubasha, Serengeti

WAZIRI Mkuu Kassimu Majaliwa amesema Serikali itashughulikia changamoto zote za kucheleweshwa kwa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ya Serengeti mkoani Mara.

Miradi hiyo ni ile inayohusu sekta ya afya, elimu, maji, barabara na kuchukua hatua kwa watakaobainika “kutafuna” fedha kutokana na uzembe, ubadhirifu  wa fedha za miradi.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo ya Februari 27, 2024 wakati akihutubia wananchi wilayani Serengeti katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa michezo mjini Mugumu kufuatia malalamiko ya mbunge wa jimbo hilo Dk. Amsabi Mrimi kwamba miradi haikamiliki kwa wakati licha ya serikali kutoa fedha.

Majaliwa amesema kuwa orodha ya changamoto zote za wilaya zilizowasilishwa kwake zitafanyiwa kazi ambapo serikali haitavumilia watumishi wanaoiharibu kwa ubadhirifu na kuwasii wananchi waendelee kuwa na imani na serikali yao wakitamani iendelee kuwahudumia.

Kauli hiyo ya waziri mkuu imekuja baada ya Mbunge wa Jimbo la Serengeti Dk. Amsabi Mrimi kupewa na fasi ya kutoa salamu za jimbo aliomba waziri mkuu kusaidia kukemea tuhuma za ubadhirifu wa fedha ka tika halmashauri zinazoletwa kwa ajili ya miradi haikamiliki wakati mwingine inakuwa chini ya kiwango.

Dk. Mrimi aliitaja miradi hiyo kuwa ni ile ya afya,barabara,maji na elimu ambapo serikali imetoa fedha nyingi kutekeleza miradi hiyo jambo la kusikitisha haikamiliki kwa wakati huku wilaya nyingine wanapewa kiasi cha fedha kama hicho miradi yao inakamilika kwa thamani ya fedha.

Alifafanua kuwa mwaka 2017 serikali ilitoa fedha kuboresha kituo cha afya Iramba Nyagasense hazijulika ni zilipo pia vituo viwili vya afya machochwe na kenyana kila kimoja kilipewa shilingi milioni 500 fedha haziku tosha na havijakamilika huku wilaya nyingine wakikamilisha kwa kiasi hicho cha fedha.

Aidha, mbunge aliendelea kulalamika kuwa kijiji cha Nyamitita kilipata mradi wa maji ya bomba serikali ilitoa fedha ni zaidi ya miaka 5 wananchi wanalalamikia mradi huo pia upo mradi wa maji miji 28 mugu mu ukiwa mji moja wapo umefika asilimia 5 ya utekelezaji  upande wa elimu ujenzi wa shule ya Sekonda ri  Moroto nga haujakamilika wakipokea milioni 500 na kueleza kuwa fedha zinavyotumika kwa wilaya hii haikubaliki.

Wabunge wa viti maalumu, Agnes Marwa aliomba serikali kujenga kituo cha magari ya abiria cha kisasa kwa ajili ya watalii pamoja na kujenga soko nzuri la kisasa katika mji wa Mugumu kwa watalii ili wananchi waweze kuuza bidhaa zilizo bora kwa ajili ya watalii wanakuja kutembelea hifadhi ya Serengeti.

Upande wake mbunge Ester Matiko akiomba serikali kujenga miundombinu ya barabara ya lami kuingia wilayani hapa ikamilike kwa wakati kwan I hifadhi ya Serengeti inaleta watalii wengi wakijengewa uwanja wa ndege kuinua uchumi wa Taifa.

Hata hivyo Majaliwa amesema sekta  zilizolalamikiwa mawaziri husika Ummy Mwalimu (afya), Dk. Festo Dugange(Tamisemi), Jumaa Aweso(maji) na wizara nyingine atawapigia simu ili waje wilayani Serengeti kushughulikia changamoto hizo haraka iwezekanavyo wananchi wasiendelee kulalamikia serikali yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles