29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 20, 2021

SERIKALI IONGEZE NGUVU KUKOMESHA UVUVI HARAMU

NA OSCAR ASSENGA

-MKINGA

KASI ya uvuvi haramu kwenye maeneo mbalimbali ya Bahari ya Hindi na Maziwa hapa nchini, imekuwa ikishika kasi kila kukicha licha ya kuwapokwa jitihada kubwa ambazo zinafanywa na Serikali kudhibiti hali hiyo.Lakini hali imeendelea kuwa si nzuri kutokana na aina ya zana ambazozimekuwa zikitumika ikiwemo mafataki, nyavu za matundu madogo na nyavuza virungu zinazodaiwa kuwa mwiba mkubwa kuharibu rasilimali zabahari.

Uvuvi huo umekuwa na athari kubwa ikiwemo kukimbiza samaki wakubwa,

jambo ambalo ni hatari kwa sekta hiyo muhimu ambayo inaweza kuingizia

Serikali mapato mengi kutokana na sera ya viwanda.

Licha ya kufanyika doria za mara kwa mara, bado mambo yameonekana kuwa magumu hasa kwenye ukanda wa Bahari ya Hindi eneo la Moa ambalo inadaiwa baadhi ya wavuvi wanatumia zana haramu kufanya shughuli zao baharini.

Jambo hilo si kwamba linaharibu mazalia ya samaki, lakini pia linasababisha kukimbiza samaki wakubwa ambao walikuwa wanategemea wale

wadogo kama chakula kwani wanapokosekana kutokana na hali hiyo

wanakimbia kwenye ukanda mwingine ulio salama na uhakika wa chakula.

Pamoja na hayo lakini pia hali hiyo inasababisha wakati mwingine

kukosekana kwa samaki ambao wanaweza kusaidia kuinua uchumi wa nchi, kwani wanapouzwa nje ya nchi huwezesha mipango ya maendeleo.

Hivyo, suala la uvuvi haramu linapaswa kuwekewa mipango kabambe

endelevu ambayo itasaidia kupambana nalo kuliko ilivyokuwa hivi sasa

ambapo mara nyingi limekuwa likisimamiwa na kamati ndogo ndogo za

Uhifadhi wa Mazingira ya Bahari na Rasilimali zake (BMU) chini ya

watendaji wa vijiji.

Licha ya kamati hizo kufanya kazi zake kwa waledi mkubwa, wavuvi

hao wamekuwa wakitumia mbinu mbadala kuhakikisha wanaingia baharini na kufanya uharibifu wa kuvua kwa kutumia zana haramu.

Mbinu wanazotumia ni pamoja na kufanya utafiti wao kubaini kama hizo zipo maeneo gani na wao wanahamia maeneo mengine kwa ajili ya kuendelea na shughuli zao.

Watu wanaweza kuona kama hizi kamati ndogo za BMU hazifanyi kazi zake ipasavyo lakini zinazidiwa maarifa, hivyo ni wajibu wa Serikali kuona namna ya kupambana na jambo hilo kwa kuweka nguvu kubwa huko ili kulitokomeza kwa mustakabali wa viumbe vya bahari .

Ili kuhakikisha suala la uvuvi haramu linakomeshwa kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini, lazima kuwepo na ulinzi shirikishi baharini kwa lengo la kudhibiti hali hiyo ambayo unaweza kusema hivi sasa limekuwa janga kubwa kwani kila mahali limekuwa likifanyika.

Kwa ushirikiano baina ya wizara husika na wilaya zilizopo pembezoni mwa Bahari ya Hindi, zingeweka mpango kabambe wa kukabiliana na tatizo hilo ili liweze kupungua kama si kwisha.

Ni wajibu wa Serikali na mamlaka husika kuona namna ya kuziwezesha kamati hizo za BMU ili ziweze kuwa na tija kubwa kwenye

maeneo yao lakini pia kuweka sheria ya kuwa atakayeshindwa kutunza

siri za kupambana na uvuvi haramu, afikishwe kwenye vyombo vya

kisheria.

Serikali kupitia wizara husika ione namna ya kusaidia doria za mara kwa mara kabla ya kutokea  uharibifu mkubwa unaofanywa na wavuvi haramu kwa kutumia zana zisizoruhusiwa kisheria.

Doria lazima ziimarishwe kila wakati ili kuondokana na uvuvi haramu

ambao umekuwa tishio kwenye ukanda wa Pwani wa Bahari ya Hindi na

hivyo kutishia usalama wa viumbe vya majini.

Kuna haja pia kwa mamlaka husika na Serikali kuangalia upya suala la uvuvi maana wapo wengine wanadaiwa kutoka nchi jirani ya Kenya ambao hawana vibali wanaingia kuvua upande wa Tanzania na hivyo kusababisha msuguano baina yao.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,579FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles