27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, December 7, 2023

Contact us: [email protected]

“Serikali iongeze kasi mabadiliko ya sheria”-TEF

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile ameiomba Serikali kuongeza kasi katika mchakato wa mabadiliko ya Sheria ya Huduma za Habari zinazominya haki ya kupata habari na uhuru wa habari. 

Balile alitoa kauli hiyo juzi Dar es Salaam wakati akizungumzana na baadhi ya waandishi wa Habari juu ya hatua iliyofikiwa baada ya wadau kuwasilisha mapendekezo ya marekebisho ya sheria hizo ambapo amemuomba Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye atimize ahadi aliyoitoa.

Alisema Waziri Nape mara baada ya kuteuliwa alikutana na wahariri, wadau na waandishi na kuahidi kuboresha sheria zinazominya uhuru wa habari ili kukuza sekta hiyo hapa nchini.

“Tangu Mei tulipopeleka mapendekezo yetu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tunaona kasi ya kuelekea kwenye marekebisho tuliyoahidiwa inazidi kupungua, hatuji ni kwanini lakini bado tuna Imani na Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali anayoiongoza, tunatamani mabadiliko hayo yafanyike mwaka huu” alisema

Balile alisema Wizara ilishaeleza kuwa itafanya mikutano na majadiliano na wadau mbalimbali ili marekebisho yatakayofanyiwa yawe na mawazo ya watu wengi lakini mpaka sasa mikutano hiyo haijafanyika kwa kasi waliyoitarajia.

Mwenyekiti huyo wa TEF alisema, mabadiliko ya sheria hizo bado ni muhimu kwa mazingira yua sasa huku akipendekeza kasi ya mabadiliko hayo ili kuwa Bunge la Novemba kwa kuwa ndio bunge la miswada.

“Bado tunazihitaji sheria, bado tunahitaji hayo mabadiliko haraka kadri inavyowezekana kuliko wakati wowote ule kwa sababu, tukipitwa na lile bunge la mwezi wa tisa, ina maana tutasubiri mwaka mmoja baadaye. Bunge la mwezi wa tisa ndio la miswada,” amesema.

Pamoja na kuchelewa huko, Balile alisema iwapo wizara yenye dhamana ikiamua kuongeza kasi katika mchakato huo, upo uwezekano mkubwa wa kufikia malengo ndani ya muda muafaka.

“Tunachotafuta zaidi ni haki ya kupata habari na uhuru wa vyombo vya Habari. Huu uhuru unawezesha haki nyingine kupatikana. Mfano demokrasia na vingine vyote vinavyozungumzwa, vinatokana na uhuru wa watu kutoa mawazo yao.

“Inapokuwa uhuru haujalindwa kisheria, basi unachelewesha hivi vingine kupatikana katika jamii. Huu ni mjadala na mchakato tunaopaswa kushirikishana tulio wengi kwa Pamoja,” amesema.

Akiwa katika Mkutano wa Wadau wa Maendeleo kusaidia ukuaji wa habari juzi Waziri Nape alisema, serikali imetoa nafasi kwa wanahabari kuwasilisha mbadala wa maoni yao na Serikali itakamilisha mchakato huo kwa muda mfupi.

“Serikali imetoa nafasi kwa wanahabari kuleta mbadala wa yale yanayolalamikiwa, tukae mezani tuzungumze na huo mchakato haiwezi kuwa mfupi, ni chakato wa mazungumzo, mie nimeukuta na tuaendelea nao. Tuna malengo ya kuukamilisha mapema kadri inavyowezekana,” alisema Nape.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles