30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wadau wa usalama waendeleza kampeni ya kutoa elimu ya usalama barabarani

Na Jeremia Ernest, Mtanzania Digital

WADAU wa usalama Barabarani nchini wameendelea na kampeni ya kuhakikisha wanafunzi shuleni wanapatiwa Elimu ya usalama barabarani ili kupunguza vifo vya ajali kwa watoto.

Akizungumza na waandishi wahabari mara baada ya kuzindua rasmi Matembezi ya kilometa 30 kwa ajili ya kuhamasisha Elimu ya usalama barabarani Mashuleni, Makamo wa Rais wa Kampuni ya Mbio za Magari (AAT) amesema wataendelea kutoa Elimu Kwa shule za Misingi na sekondari katika wilaya ya ilala na nyingine Ili kuhakikisha watoto wanafikia ndoto zao Kwa kuepuka ajali zisizo za lazima.

“Tutaendelea kushirikiana Kwa karibu na wadau mbalimbali wa usalama Barabarani kuhakikisha tunatoa elimu pamoja na vifaa vitakavyowezesha watoto mashuleni kuvuka barabara Kwa usalama zaidi.”

Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi na Afisa mnadhimu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, ACP Meloe Buzema amesema endapo watumiaji wa barabara wataendesha kwa kasi ya kilomita 30 kwa saa hususani katika maeneo masoko, Shule, Hospital na nyumba za ibada itasaidia kwa asilimia kubwa kupunguza ajali za barabarani.

kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaam wakati alipokua katika Semina iliyoandaliwa na Chama cha Mashindano ya magari ya AAT ya kuwajengea uwezo wanafunzi wa shule ya msingi na Sekondari mnazi mmoja yenye lengo la kupunguza kasi ya uwendeshaji kutoka kasi ya kilomita 50 hadi 30 kwa saa.

Amesema kuwa, elimu iliyotolewa kwa wanafunzi hao itafika sehemu nyingi zaidi kwani watoto hao watakua mabalozi wazuri wa kutoa taarifa kwa jamii tofauti na kuzungumza kwenye vyombo vya habari kwani sio wote ambao wataweza kuona taarifa hiyo, hivyo kitendo kilichofanywa na Chama cha hicho ni mfano wa kuigwa na kwa wadau wengine.

“Jambo walilolipendekeza wenzentu hawa wa AAT ni zuri sana, kwani kuendesha kwa kasi ya 30 itapelekea barabara zetu kuwa salama zaidi kwani hata ikitokea kuna ajali imetokea haiwezi kuleta athari kubwa kutokana na mwendo uliotumika tofauti na mwendo kasi”.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Chama cha Mashindano ya magari (AAT) Najma Rashid amesema kuwa, wanategemea kuongeza uwelewa katika masuala ya usalama barabarani kupitia miradi yao na kufikia lengo la kupunguza ajali kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2030.

Aidha, amesema kuwa, wataendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo walimu wa shule za msingi na Sekondari, jeshi la Polisi pamoja na wanafunzi katika kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya barabara na kuepuka ajali zisizo za lazima lengo ikiwa ni kuhakikisha wanaweza kupunguza kasi ya uwendeshaji kutoka kilomita 50 kwa saa jadi kufikia kilomita 30.

Ameongeza kuwa, endapo kutakua na usimamizi mzuri wa kasi za uendeshaji kwa madereva barabarani itakua ni njia mbadala wa kuokoa maisha na majereha ya kudhoofisha kwani Uhusiano mkubwa kati ya mwendokasi na kifo hutumika na watumiaji wote wa barabarani.

Naye, Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Saady Khimji ameikipongeza chama hicho kwa kushirikiana na Taasisi za Serikali katika kuhakikisha wanatoa elimu ya usalama barabarani pamoja na kutoa vifaa mbalimbali vya usalama barabarani.

“Sisi kama Serikali, tunatambua mchango mkubwa unaofanywa na chama cha Mashindano ya Magari (AAT) kwani wamekua wakitoa elimu ya usalama na kupelekea kupungua kwa ajali za barabarani tofauti na miaka ya nyuma, tunaomba na wadau wengine waweze kuiga mfano wao Ili tuhakikishe ajali za barabarani zinapungua,” amesema Khimji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles