25.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali inazitambua Asasi zote za kiraia kwa kazi nzuri-Dk. Gwajima

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Doroth Gwajima amesema Serikali inazitambua Asasi zote za Kiraia kwa kazi nzuri zinazofanya kwa ajili ya manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla.

Dk. Gwajima ameyasema hayo Alhamisi Oktoba 28, wakati akitoa tuzo mbalimbali kwa baadhi ya Asasi za Kiraia zilizofanya vizuri zaidi katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma baada ya kumalizika kwa wiki ya AZAKI.

Amesema Asasi zote zinafanya vizuri lakini Tuzo hizo zimetolewa kwa wale walionesha ubunifu na kujitolea zaidi katika utendaji kazi zao katika kuhakikisha wananchi wanafaidika na miradi wanayoiendesha katika Mashirika yao.

“Tunapoikuza jamii yetu ya Kitanzania tunamsaidia Rais Samia Suluhu Hassan kutekeleza maono yake kwenyeTaifa hili na nipende kumshukuru kwa maono yake amekuwa akihamasisha tuzidi kuimarisha ushirikiano na Asasi za Kiraia, amesema Dk. Gwajima.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dk. Jingu ameipongeza AZAKI kwa midahalo iliyofanyika katika wiki yote ambayo ina lengo la kuimarisha utekelezaji wa majukumu yao na kufanya tathmini ya kuboresha katika utekelezaji wa majukumu hayo. 

“Nyie kama Wadau wa Maendeleo mkaoneshe kweli kuwa nyie ni wadau kwa kulenga kuleta matokeo zaidi na kubuni namna ya kupata Rasilimali kwa ajili ya kuendeleza shughuli zenu,” amesema Dkt. Jingu.

Amesema Wizara itaendelea kutoa ushirikiano kwa Asasi zote za Kiraia ikiwemo utoaji ya miongozo mbalimbali na kuwahimiza waendelee kufanya kazi kwa bidi kwa kuzingatia Sheria, taratibu na kanuni zilizopo.

Naye Rais wa Asasi za kiraia Dk. Stigmata Tenga ameishukuru Serikali kwa kuthamini mchango wa AZAKI na kuwapa nafasi katika kuchangia maendeleo ya Taifa kupitia miradi mbalimbali inatotekelezwa na Asasi hizo katika maeneo tofauti nchini.

“Wizara imekua ikionesha kutusikiliza na kukaribisha mawazo yetu hivyo kututia moyo zaidi kuendelea kufanya kazi,” amesema Dk. Tax.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles