24.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

Bilioni 22 kuboresha barabara Kagera

Na Renatha Kipaka, Bukoba

Kiasi cha Sh bilioni 22 imetolewa kwa ajili ya ujenzi wa barabara mkoani Kagera ambapo kwa mwaka huu ikiwa ni ongezeko la Sh bilioni 9 kwa mwaka huu.

Hayo yamebainishwa Alhamis Oktoba 28, 2021 na Mkuu wa Mkoa Kagera, Meja Jen. Charles Mbuge wakati alipozindua utiaji saini kwa Makandarasi mbalimbali mjini Bukoba.

Jen. Mbuge amesema serikari ya Rais Samia Suluhu Hassan ameona umuhimu wakuongeza fedha za barabara ili iwe rahisi kuwasiliana kwa karibu na wezesha wanchi kufanya biashara zao kwa urahisi na kukuza uchumi.

“Nitumie nafasi hii kuwaeleza nyie wakandarasi kuwa mimi huwa napenda uwazi hasa katika utendaji kazi, watu wanapopewa kazi wakati hawana uwezo nisingependa itokee nibora wewe uache mwenyewe kuliko kuharibu,” amesema Mbunge.

Kwa upande wake Injinia wa Tarura, Aviti Theodory amesema katika utiaji saini ni mikataba 23 pekee iliyosainiwa kwa ajili ya kuanza kazi.

“Niseme tu katika hatua hii ya utiaji saini kwa wakandarasi na akina mama wamepewa kipaumbele kwa tenda ambazo nikazi za kutumia mikono ili kuonyesha usawa japo nao wanatakiwa kufanya kazi kwa ubora,” amesemaInjinia Theodory.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles