27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Ummy ahitimisha Wiki ya Asasi za Kiraia akiahidi serikali kutoa ushirikiano

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ummy Mwalimu ameshiriki hafla ya kuhitimisha Wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) jijini Dodoma.

Katika hotuba yake mbele ya Wadau wa Serikali na Mashirika ya Asasi za Kiraia nchini ameahidi kutoa ushirikiano kwa mshirika hayo na kuyasihi kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi ikiwa ni moja ya mchango mkubwa wa maendeleo ya nchi.

“Kwa kutambua mchango wa Azaki natoa wito kwenu kuendelea kushirikiana na Serikali kuendelea kuihudumia jamii ambayo Asasi hizi mmekuwa mkifanya kazi nizuri kwa kuifikia jamii hasa wananchi walioko vijijini kwa kushirikiana na serikali za Vijiji na halmashauri,” amesema Ummy.

Aidha, ametoa wito kwa Sekta Binafsi kuwekeza kwenye mashirika ya Asasi za Kiraia ili kuchangia ukuaji wa maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla na kwamba kwa kufanya hivyo kutaisaidia Sekta Binafsi  kutimiza malengo yao ya huduma za jamii kwani asasi hizo zimekuwa zikifanyakazi na jamii hizo kwenye maeneo yao.

Pia amezitaka Asasi za Kiraia kuongeza nguvu katika suala zima la kutoa elimu kwa wananchi na kuwajengea uwezo ili wananchi hao waweze kujisimamia katika shughuli zao za kimaendeleo na kiuchumi huku akiwataka kuwasaidia madiwani kwenye halmashauri kwa  kuwajengea uwezo kwenye masuala mbalimbali yakiwemo usimamizi wa fedha na miradi ya maendeleo.

Napenda kuwapongeza sana kwa elimu mnayotoa kwa wananchi kwa kuwajengea uwezo, lakini naomba muende mbali zaidi kuyafikia mabaraza ya madiwani kwenye halmauri zetu ili nao wajengewe uwezo wa kusimamia halmashauri kwenye matumizi ya fedha na ufuatiliaji wa shughuli za maendeleo,” ameongeza Ummy.

Awali akitoa Salamu na kuelezea shughuli mbalimbali zilizofanywa na Asasi ya Kiraia kwenye Wiki ya Azaki, mratibu wa Wiki ya Azaki na Mshauri wa Foundation for Civil Society (FCS) Justice Rutenge ameeleza kazi zilizofanywa katika wiki ya Azaki ikiwa ni pamoja na mijadala mbalimbali iliyowakutanisha wadau wa Asasi za Kiraia, Wabunge, Makundi Maaalum na wananchi ambapo kwa pamoja waliweza kushirikiana katika mazungumzo na mijadala iliyolenga kujadili masuala yanayohusu  ustawi wa  nchi na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

“Mheshimiwa Waziri Wiki ya Azaki mwaka huu imeweza kuzikutanisha Asasi zaidiya 300 ambao kwapamoja waliweza kukutana hapa Dodoma kuanzia siku ya ufunguzi na baadae kushiriki kwenye mijadala mbalimbali iliyowawezesha kutoa mawazo yao juu ya masuala mbalimbali ya ustawi wa jamii na Taifa kwa ujumla,”amesema Justice.

Wiki ya AZAKI ni jukwaa pekee nchini lililowaleta kwa pamoja  wadau wakuu wa maendeleo  ikiwemo Serikali, Sekta Binafsi na Asasi za Kiraia,  pamoja na wananchi kwa lengo la  kujadili masuala yanayohusu  ustawi wa  nchi na maendeleo ya Taifa ambapo yalizinduliwa rasmi leo Oktoba 23 na Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, na kufungwa rasmi Oktoba 28, 2021 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles