23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali iko imara, Watanzania endeleeni kuiamini- Majaliwa

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Waziri Muu Kassim Majaliwa amesema Serikali ipo imara na miradi yote ya kimkakati inaendelea kujengwa, hivyo Watanzania waendelee kuwa na imani nayo.

Amesema Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ipo makini na inaendelea kuwatumikia Watanzania. ”Tuendelee kuchapa kazi”.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne, Aprili 20, 2021) baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota, Dar es Salaam.

”Siri ya kuwepo mafanikio na maendeleo nchini ni utulivu na amani. Tulianza vizuri tangu Serikali ya Awamu ya kwanza, tutaendelea kuimarisha amani na utulivu,”amesema Majaliwa.

Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwaasa Watanzania watumie muda mwingi kufanya shughuli za maendeleo kuliko mambo mengine yasiyo na tija.

Akizungumzia kuhusu mradi huo, Majaliwa amesema amefurahi kukuta majengo yamekamilika na kwamba ameridhika na maendeleo ya ujenzi wake.

Aidha, Majaliwa ameuagiza uongozi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wahakikishe wanakamilisha kazi iliyosalia haraka ili mwaka huu wananchi waanze kuishi hapo.

Naye, Mtendaji Mkuu wa TBA, Daud Kondoro amesema mradi huo una jumla ya block tano na ambazo zinauwezo wa kuchukua familia 656.

Amesema mbali na ujenzi wa nyumba hizo za makazi pia katika eneo hilo wanajenga maduka makubwa pamoja na vizimba kwa ajili ya wajasiriamali kufanya biashara.

Mradi ulianza kutekelezwa mwaka 2016 na unatarajiwa kukamilika Mei 2021. Hadi sasa umefikia asilimia 94 ya utekelezaji wake na gharama yake ni shilingi bilioni 50.

Baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za makazi za Magomeni Kota, Waziri Mkuu alikagua kituo cha Reli ya Kisasa cha Tanzanite jijini Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles