22 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

Rais Chad afariki dunia, Waasi wahusika

N’Djamena, Chad

Rais wa Chd, Idriss Déby Itno, amefariki akiwa na umri wa miaka 68, chanzo kikitajwa kuwa ni majeraha aliyopata akikabiliana na waasi.

Deby Itno aliyeiongoza Chad kwa miaka 30, alijeruhiwa wakati akiliongoza jeshi katika mapambano dhidi ya waasi Kaskazini mwa nchi hiyo.

Aliyetangaza taarifa ya kifo cha rais huyo ni Msemaji wa Jeshi, Jenerali Azem Bermandoa Agouna.
“Ni huzuni sana na inauma kuwatangazia watu wa Chad kifo hiki cha Kiongozi wao leo Jumanne ya Aprili 20, 2021,” amesema Jenerali Agouna.

Msemaji wa jeshi la Chad amesema Rais Idriss Deby amefariki dunia. 

Kupitia matangazo ya televisheni ya umma wa taifa hilo, msemaji  wa jeshi, Agouna amesema kwamba baraza la kijeshi limemchagua mtoto wa kiongozi huyo, Mahamat Kaka, kuwa rais wa mpito.

Tangazo la kifo chake limetokea saa chache tu baada ya Deby kutangazwa mshindi wa uchaguzi kwa kupata asilimia 79 ya kura licha ya wapinzani wake wakuu kuamua kususia uchaguzi huo wa Aprili 11.

Waziri mkuu wa zamani, Albert Pahimi Padacke ameshika nafasi ya pili katika kinyang’anyiro hicho kwa kupata asilimia 10.32 tu, na idadi ya waliojitokeza ilikuwa asilimia 64.81, kwa mujibu wa takwimu za awali zilizotangazwa na mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Kodi Mahamat Bam.

Matokeo hayo yalitangazwa baada ya jeshi kufanya mazoezi kwenye mitaa ya mji mkuu, N’Djamena. Kwa ushindi huo, Rais huyo mwenye umri wa miaka 68 angeiongoza nchi hiyo kwa muhula wa sita mfululizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,284FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles