22 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

SERIKALI: HAIWEZEKANI MAJUTO KUOMBA SH 500,000


Gabriel Mushi, Dodoma    |   

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amesema inaudhi kuona msanii wa filamu, Amri Athuman maarufu King Majuto anaomba msaada wa Sh 500,000 kwa ajili ya matibabu wakati kuna makampuni yalifaidika naye kwa kuingia mikataba aliyodai ya dhuluma.

Kutokana na hali hiyo, amesema serikali imechoka kusikia vilio vya wasanii wa filamu kudhulumiwa haki zao na sasa imeunda kamati maalumu ya wanasheria kukagua mikataba yote ya mashirika na makampuni waliyoingia wasanii akiwamo  King Majuto na marehemu Seteven Kanumba ‘Kanumba’.

Pia imeagiza wasanii wote ambao wanaona wameingia mikataba ya kipumbavu na makampuni au mashirika hayo wawasilishe taarifa zao kwa serikali.

Dk. Mwakyembe amesema hayo leo Aprili 27, bungeni jijini Dodoma wakati akijibu hoja za wabunge katika kuhitimisha hotuba ya bajeti ya wizara hiyo.

“Kwa kweli dhuluma kwa wasanii ilikuwapo kubwa sana kwa kutumia ‘middle men’ (watu wa kati), watu wenye fedha wamechezea sana Watanzania wetu. Hili limeanza kubadilika tumeanza kuwa- empower (kuwezesha) wasanii wetu kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) wasitumie middle men.

“Kwa mfano vijana wetu wazuri kama kina Kanumba, amefariki kila mtu anajua ni milionea, hapana.. waliotajirika ni wengine. Leo hii mwanasanaa mzuri mzee majuto anaumwa, anaomba fedha, mimi nachanga kutoka mfuko kwangu,” amesema Dk. Mwakyembe.

Amesema licha ya kwamba nusu ya mabango ya biashara na matangazo ya biashara ni ya  Mzee Majuto inashangaza kuona anaomba fedha ya matibabu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,284FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles