BUENOS AIRES, Argentina
MKURUGENZI Mkuu Mtendaji wa wa Mfuko wa Uwekezaji nchini hapa (RDFI), Kirill Dmitriev amesema takribani dola bilioni moja kutoka mfuko wa pamoja baina ya nchi hii na Saudi Arabia zitatumika kwa ajili ya kuboresha miundombinu kuanzia mwakani.
Mkurugenzi huyo alitoa taarifa hiyo jana katika alipozungumza na waandishi wa habari akisema tayari wenzao wa Saudi Arabia wamethibitisha nia yao ya kuwekeza katika miradi ya miundombinu nchini hapa.
“Saudi Arabia wameshathibitisha nia yao ya kushiriki katika uwekezaji katika miradi kadhaa ya miundombinu ambayo iliwasilishwa na RDIF na miaka mingine ijayo tunapanga kuwekeza dola nyingine bilioni mbili kutoka katika mfuko wa pamoja wa Urusi na Saudi Arabia,”alisema Dmitriev.
Alifafanua kwamba miradi 12 ilipendekeza na mfuko wake huo na yote itaanza kufanyiwa kazi.
Dmitriev alisema miongoni mwa mambo yaliyozungumzwa kwenye mkutano baina ya kiongozi wa nchi hii, Vladimir Putin na Mfalme wa Saudi Arabia, Prince Mohammed bin Salman ni kuhusu nchi hiyo kuongeza uwekezaji nchini hapa.
Alisema matunda ya uwekezaji wa Saudi Arabia nchini humu yameshaanza kuonekana.
“Miaka miwili iliyopita uwekezaji wa Saudi Arabia ulikuwa hauna kitu, lakini sasa umeshazaa zaidi ya dola bilioni mbili,” alisema Dmitriev.