26.1 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Sare za wanasiasa ni zaidi ya mavazi

Na ALOYCE NDELEIO

WAKATI kampeni za vyama vya siasa kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika leo zikiwa zimekwisha, yamekuwapo mambo mengi ya kuvutia lakini mojawapo kubwa ni kutamalaki ni mavazi ambayo ni sare.

Sare hizo zimevaliwa na wagombea wa nafasi mbalimbali kuanzia wagobea wa kiti cha urais, wabunge, madiwani na hata wanachama wa vyama.

Vyama vya siasa vina utambulisho wake wa mavazi na ambayo wanasiasa wamekuwa wakiyatumia kujitambulisha au kuwasiliana na hali hiyo imefanya viongozi wengi wa Afrika kuwa na uhusiano na aina mbalimbali za fasheni.

Licha ya kwamba matokeo makubwa kuliko ilivyo katika maisha, wanasiasa wana- bakia kuwa ni binadamu. Fasheni ni muhimu kwa tabaka la kisiasa kutokana sababu mbalimbali. Sababu hizo zinajumuisha kuboresha haiba au kipaji (Charisma), kujipenyeza katika heshima na kutambulika na kuzuia au kuvuta mwonekano.

Fasheni pia ni eneo lenye faida kubwa ambalo jamii inaweza kupitia au kutazama na hata kufanya uamuzi wa kutumia. Thamani au mvuto wa baadhi ya wanasiasa huwekwa wazi chaguzi zao za fasheni.

Bereti nyekundu ni mojawapo ya fasheni ya kisiasa Afrika. Aina hii ya kofia ilitokana na mvuto wa Che Guevara na Thomas Sankara na imekuwa inavaliwa na wanasiasa wa Afrika katika kampeni zao za kutaka mapinduzi.

Wanasiasa kama Julius Malema wa chama cha EFF nchini Afrika Kusini amekuwa akitumia aina hiyo ya kofia pamoja na mavazi ya rangi hiyo. Vivyo hivyo Bobi Wine wa Uganda bereti nyekundu ni utambulisho na fasheni ya chama chake.

Fasheni nyingi za kisiasa zilianza baada ya ukoloni ambapo wanasiasa walizitumia kuonesha umaarufu wao kama si kuonesha kujitawala na kuondokana na kutawaliwa.

Wapo viongozi ambao kila wanapotokeza hadharani wanakuwa wamevalia fasheni za kisasa na za anasa wakiwemo Paul Biya wa Cameroon pamoja na familia yake.

Hata hivyo fasheni ya kuvaa miwani nyeusi (za jua) hadi kuwa moja ya vifaa pendwa lipo kwa wanasiasa na mfano halisi ni aliyekuwa kiongozi wa Libya Muamar Gaddafi, Rais wa Togo Gnassingbé Eyadéma na kiongozi wa Nigeria Sani Abacha.

Rais wa kwanza mwanamke barani Afrika Ellen Sirleaf Johnson naye alipokuwa ma- darakani hakuacha kutokeza hadharani akiwa amevalia sare ambazo zilivutia wengi.

Katika kampeni zinazoendelea hivi sasa fasheni ni taswira iliyotawala ambapo kila chama kimekuwa na mavazi ambayo yamekuwa ni utambulisho unaovutia na yeyote anayeonekana kuvaa mavazi hata kama si mwanachama au mfuasi anahesabika kufungamana navyo.

Lakini hiyo si hoja, hoja ni kwamba utambulisho huo umekuwa unafungamanisha na sera za chama na hata kutambulisha kwa wanachama na wanasiasa kuwa damu zao zina rangi ya fasheni hizo.

Pamoja na hali hiyo kuibuka na kuvaliwa kwa fasheni hizo katika msimu huu wa kampeni kunafungamanisha na sera za kiuchumi kwamba zimekuwa ni kitega uchumi kikubwa na biashara inafanyika kwa kuwa ubunifu wa fasheni hizo umekuwa ni wa ‘mlipuko’.

Hata hivyo hakuna jambo ambalo halina mkondo wa kihistoria, ndio maana baada ya uhuru wa nchi nyingi za Afrika viongozi wengi walitumia nafasi ya mavazi kuutambulisha uhalisia wa mataifa hayo na hilo lilianzia kwa kuwataja wachache Kwame Nkrumah wa Ghana na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Viongozi hawa wawili katika picha zao kwa nyakati tofauti walivaa vitenge wakimaanisha wapo Kiafrika zaidi na lengo likiwa pamoja na kuwapo fasheni za kigeni Waafrika walikuwa na wanazo fasheni zao.

Mbali na kuingia katika siasa, fasheni hizo ni muhimu na zinaonekana miongoni mwa nchi za Afrika Magharibi hadi sasa.

Baadaye, nguvu ya fasheni za kisiasa ziliingia katika jamii Tanzania hasa kipindi ambacho Mwalimu aliamua kuvaa fesheni ya suti isiyo na kola, jambo ambalo lilipenyeza mara moja miongoni mwa viongozi wa serikali na hata shuleni.

Hadi leo wapo viongozi ambao wanapojaribu kuonesha fikra zao kuhusu uongozi wa Mwalimu Nyerere hupendelea kuvaa aina hiyo ya fasheni.

Pamoja na hali hiyo yote, jambo linaloleta mvuto hususani nyakati hizi za kampeni ni kuhuishwa kwa mvuto wa fasheni na jinsi zilivyo na nguvu katika kuibadilisha mielekeo na mitazamo ya serikali.

Hali hiyo inatokana na sababu kuwa fasheni na aina ya uongozi kwa wanasiasa wa Afrika unahifadhi mambo mengi ambayo yana tija. Picha inayotolewa na fasheni za wanasiasa kunaweza kuonesha ni namna gani hujuma zipo au kutokuwepo ndani ya serikali. Lakini pia kunawezza kuonesha hitaji lililo muhimu au la na ambalo halina madhara katika chaguzi.

Hata hivyo, muhimu zaidi ni kwamba wanasiasa wanaweza kutumia fasheni hizo kama jukwaa la propaganda katika kuwavutia wanachama, wafuasi na umma kwa ujumla na hivyo kuwa zaidi ya mavazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,734FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles