29.7 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

SAMIA AWAAHIDI TREKTA WAKULIMA WA MPUNGA

Na MWANDISHI WETU-ZANZIBAR


MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan,  ameahidi kuwapatia trekta moja wakulima wa Mkoa wa Mjini Magharibi visiwani Zanzibar ili liweze kuwasaidia kuendesha shughuli zao za kilimo kwa wakati.

Hayo aliyasema jana mjini hapa, alipotembelea mradi wa wakulima wa mpunga katika Bonde la Kizimbani lililopo Wilaya ya Magharibi A Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Makamu wa Rais ambaye ameanza ziara ya siku nne ya kuhamasisha shughuli za maendeleo ya CCM Zanzibar, aliwataka viongozi na wanachama wote wa CCM kushirikiana na kudumisha amani ya nchi.

“Ni vema wakulima na wananchi wote mtambue kwamba mjenga nchi ni mwananchi, ni vema viongozi wote muwe mstari wa mbele kwenye shughuli za kuleta maendeleo na kushirikiana bega kwa bega na wananchi,” alisema Samia.

Pamoja na kutembelea shamba hilo la mpunga pia alisimamia zoezi la upandaji mpunga na kutembelea eneo la Fuoni Kibaoni ambao alishuhudia upandwaji wa miti ya mikoko ikiwa sehemu ya utunzaji wa mazingira pamoja na uzalishaji wa Kaa.

Katika ziara hiyo Makamu wa Rais aliandamana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk. Abdalla Juma Mabodi, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud pamoja na viongozi wengine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles