27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

Samia aipa Zambia zawadi ya Uhuru

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania itatenga eneo la ekari 20 katika mMoa wa Pwani kwa ajili ya kuhudumia mizigo kutoka Zambia.

Rais Dk. Samia alitoa kauli hiyo wakati akitoa hotuba kwenye maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Zambia ambapo yeye alikuwa mgeni rasmi.

Zambia ni mteja mkubwa wa bandari ya Dar es Salaam, ikichukua asilimia 34 ya mizigo yote inayopitia bandari hiyo kwenda nje ya Tanzania.

Rais Samia alitumia fursa hiyo kusema kwamba mipaka ya kijiografia baina ya Tanzania na Zambia haipaswi kuwa kikwazo cha biashara na uwekezaji baina ya nchi hizo jirani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles