23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Samatta ashangazwa kuhusishwa AS Roma

NA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAM

NAHODHA wa timu ya soka Tanzania ‘Taifa Stars’ anayekipiga katika klabu ya K.R.C Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta, ameshangazwa na taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa anatakiwa kujiunga na AS Roma ya Italia kwa majaribio.

Jana mitandao mbalimbali ya kijamii nchini ilisambaza taarifa kuwa mshambuliaji huyo aliyeichezea klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kabla ya kutua K.R.C Genk, leo anaweza kusafiri kwenda jijini Rome, Italia kufanya makubaliano ya kusaini mkataba wa kuichezea AS Roma.

Samatta nyota yake iling’ara zaidi baada ya kushinda tuzo ya kuwa mchezaji bora Afrika kwa wachezaji wa ndani Januari 7, mwaka huu.

Wakala wa straika huyo, Jamal Kisongo, aliliambia MTANZANIA jana kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote na kudai kwamba Samatta anaendelea kufanya mazoezi na timu yake ya Genk kwa maandalizi ya Ligi Kuu msimu ujao.

“Baada ya kusikia taarifa hizi nilizungumza na Samatta mwenyewe ambaye naye alielezea kushangazwa sana. Pia wakala wake wa kimataifa, Nicholas Onisse raia wa Senegal alikanusha kuwepo kwa jambo hilo,” alisema Kisongo.

Pia mshambuliaji huyo tegemeo kwa Taifa Stars alikuwa miongoni mwa wafungaji bora wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kuifungia timu yake ya TP Mazembe iliyotwaa ubingwa mabao saba sawa na Bakri Al- Madina wa El Merreikh ya Sudan.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles