24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

Simba yamuathiri Kessy kisaikolojia

NA WINFRIDA NGONYANI, DAR ES SALAAM

MENEJA wa beki wa Yanga, Ramadhani Hassan ‘Kessy’, Athumani Tippo, amesema suala la Simba kukataa kutoa barua ya ridhaa kwa beki huyo kuitumikia Yanga limemuathiri kisaikolojia.

Kessy ambaye amesajiliwa na Yanga, ameshindwa kuichezea timu hiyo katika mechi mbili za hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho, kutokana na Simba kugoma kujibu barua ya Yanga kumthibitisha kumalizika kwa mkataba wake jambo ambalo lingempa ruhusa ya kushiriki michuano hiyo.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Tippo alisema suala hilo limemuathiri mchezaji huyo kisaikolojia, akieleza ni hatari kwa mchezaji mzuri kama yeye.

“Watu hawajui tu suala hili linamuathiri sana Kessy ukizingatia ni mchezaji mzuri, sasa anapokaa bila matumaini kwa kweli wanamharibia sana, wamuache kijana, hawamkomoi yeye tu ila soka la Tanzania kwa ujumla, kwa staili hii hatuwezi kufika,” alisisitiza Tippo.

Aidha, Tippo alisema licha ya suala hilo kufika kwa Chama cha Wanasoka Tanzania (Sputanza), bado mambo si shwari  na kuzitaka  klabu zote za Simba na Yanga,  kuacha kufanyiana jeuri kwa kile alichodai kuwa imekuwa kawaida yao kufanyiana hivyo.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Selestine Mwesigwa, limesema kuwa wameamua kulifikisha suala hilo kwenye Kamati ya Sheria na hadhi ya wachezaji ili kulitolea maamuzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles