27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mkutano Simba wasogezwa mbele

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

MKUTANO Mkuu wa wanachama wa klabu ya soka ya Simba uliopangwa kufanyika Julai 10, mwaka huu katika Ukumbi wa Maofisa wa Polisi Masaki, jijini Dar es Salaam, umesogezwa mbele hadi Julai 31, mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Rais wa klabu hiyo, Evans Aveva, ilieleza kwamba  uamuzi wa kuahirishwa kwa mkutano huo umetokana na sababu kubwa ya uongozi kutaka kuwajibika zaidi kwa upande wa timu inayojiandaa na michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Alisema uongozi umefanya mabadiliko hayo uweze kuelekeza nguvu zake kukiandaa kikosi kwa ajili ya mazoezi.

“Tunaomba radhi kwa wanachama kutokana na usumbufu uliojitokeza, lakini tunakiri kwamba mambo haya yanafanywa ili kuongeza ufanisi ndani ya klabu yetu,” ilieleza taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles