Sam Hamisi aachia ‘Tenda Wema’

MICHIGAN, MAREKANI

MWIMBAJI wa Injili kutoka nchini Marekani, Sam Hamisi Luc, amewaomba wapenzi wa muziki huo kusikiliza kwa makini ujumbe uliopo kwenye wimbo wake mpya, Tenda Wema.

Akizungumza na MTANZANIA hivi karibuni, Sam alisema wimbo huo ambao umetoka wikiendi hii, umebeba ujumbe unaotoa hamasa kwa jamii kutendeana wema kila wakati.

“Nimeachia wimbo wangu mpya unaitwa Tenda Wema, natamani kila mmoja ausikilize ili apate ujumbe ambao una hamasisha watu wa Mungu kutendeana wema, video tayari nimeiweka kwenye chaneli yangu ya YouTube naomba sapoti,” alisema Sam.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here