31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Marekani yapeleka vikosi zaidi Syria baada ya kuzozana na Urusi

WASHINGTON, MAREKANI

MAMIA kadhaa ya wanajeshi wa Marekani wamesalia kaskazini mashariki mwa Syria huku idadi nyingine ikiongezwa.

Marekani imeongeza idadi ya wanajeshi wake Syria baada ya malumbano kati yake na Urusi kuzua hali ya taharuki nchini humo.

Maofisa wa Marekani wamesema magari sita ya vita na karibu wanajeshi 100 wamepelekwa kaskazini mashariki mwa Syria.

Visa vya makabiliano kati ya vikosi vya Marekani na Urusi vinavyoweka ulinzi katika nchi hiyo vimeongezeka mwaka huu.

Kapteni wa jeshi la majini la Marekani Bill Urban amesema hatua hiyo itasaidia kuhakikisha usalama wa vikosi vya muungano.

Ameongeza kuwa, pamoja na magari hayo ya vita ambayo yalikuwa Kuwait, Marekani pia itapeleka vifaa vya ulinzi wa angani na kuongeza doria za mara kwa mara zinazofanywa dhidi ya vikosi hivyo.

“Marekani haina mpago wa kuzozana na nchi nyingine Syria, lakini italinda vikosi vya muungano ikilazimika kufanya hivyo,” Urban, ambaye ni msemaji wa majeshi ya Marekani alisema, katika taarifa siku ya Ijumaa.

Urban hakutaja Urusi kwa jina, lakini katika taarifa nyingine kutoka kwa maofisa wa Marekani, iliyoangaziwa kwanza na kituo cha habari cha NBC, aliashiria anazungumzia nchi hiyo.

“Hatua hii inatuma ishara kwa Urusi kujiepusha na vitendo vya uchokozi kaskazini mashariki mwa Syria,” alisema ofisa mmoja ambaye jina lake halikutajwa.

Kituo cha NBC kiliwanukuu maofisa hao wakidaiwa kusema kwamba wanajeshi zaidi na magari ya kivita yamepelekwa kaskazini mashariki mwa Syria ili kuzuia vikosi vya Urusi kuingia katika maeneo ya usalama ambako vikosi vya Muungano vya Marekani  na vikosi vya Kikurdi vinaendesha oparesheni.

Kwa miaka kadhaa sasa, kumeshuhudiwa mzozo wa mara kwa mara kati ya vikozi vya Marekani na Urusi nchini Syria. 

Lakini matukio ya wiki za hivi karibuni kaskazini mashariki mwa Syria vimeongeza uhasama kati ya nchi hizo mbili.

Mwisho wa mwezi Agosti, wanajeshi saba wa Marekani walijeruhiwa baada ya gari lao kugongana na gari la kijeshi la Urusi. 

Serikali za Urusi na Marekani zililaumiana kufuatia tukio hilo ambalo lilinaswa kwenye kanda ya video na kuwekwa katika mtandao wa kijamii wa Twitter.

Video hiyo inaonesha gari la kijeshi la Urusi katika msafara wa jangwani likigongana na gari la kijeshi la Marekani, Helikopta ya Urusi ilipaa umbali wa chini kabisa.

Urusi inasema kuwa Marekani ilizuia doria.

Marekani ilisema Urusi iliingia katika ‘eneo la usalama ambalo walikuwa wamekubali hawatafika.

Urusi kwa upande wake inasema kuwa ilitoa taarifa mapema kwamba vikosi vyake vitafanya oparesheni katika eneo hilo

Picha inayoonesha makabiliano hayo iliwekwa kwenye tuvuti ya Urusi ya Rusvesna.su

Marekani ina karibu wanajeshi 500 katika eneo hilo – ambao ni wachache ikilinganishwa na idadi ya awali iliyokuwa hapo- kusaidia kuweka ulinzi na kuvunja tishio lolote kutoka kwa wanamgambo wa kijihadi wa kundi la Islamic State.

Kumekuwa na matukio kadhaa yanayohusisha wanajeshi wa Marekani kaskazini mwa Syria. 

Wiki kama moja hivi iliyopita ilikuwa na makabiliano makali na Urusi, washirika wa Syria.

Februari 2018, kundi kubwa la mamluki la jeshi la Urusi lilizindua mashambulio dhidi ya eneo la Marekani karibu na eneo kubwa la mafuta na wanajeshi wake wakapata majeraha.

Ingawa tukio hilo la hivi karibuni ni tofauti kidogo. Chanzo chake ni makabiliano ya moja kwa moja kati ya maofisa wa jeshi wa Urusi na vikosi vya Marekani. 

Marekani inasisitiza kwamba hilo ni sehemu ya matukio ambayo yamekuwa yakitokea. 

Urusi inaiona Marekani kama inayokaribia kuondoka Syria. Oktoba mwaka jana, Rais wa Marekani Donald Trump aliamua kuondoa wanajeshi 1,000 ambao walikuwa wakiunga mkono muungano wa Kikurdi, lakini akabadilisha mawazo yake na kubakisha wanajeshi kidogo katika eneo ambalo limewekewa masharti mengi.

Lakini Urusi inafahamu kwamba Trump anataka kupunguza wanajeshi wa Marekani nje ya nchi na vilevile, inaonekana kutaka sana Marekani ijiondoe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles