31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Sababu za Kiba kumrudisha kwao mkewe hizi hapa

SWAGGAZ RIPOTA

HATIMAYE mfalme wa Bongo Fleva Ali Kiba, amevunja ukimya kwa kujibu tetesi zilizozua gumzo wiki hii kuhusu kumchapa talaka tatu mkewe Amina Khalef (mama Keyaan) na kumrudisha kwao Mombasa Kenya.

Hivi karibuni Kiba, alijibu maswali yote  aliyoulizwa na mtangazaji Diva The Bawse kuhusu ndoa yake hiyo iliyofungwa mwaka jana jijini Dar es Salaam na sherehe kubwa ikafanyika hoteli ya Serena.

JE MKEWE HAWAPENDI NDUGU ZAKE?

Katika mitandao ya kijamii wiki hii, kumekuwa na picha mbalimbali za utani zinaoonyesha watu wengi wakiwa eneo moja na kusema watu hao ni ndugu wa Ali Kiba wanapokuwa nyumbani kwa msanii huyo.

Huku wengine wakidai mke wa Ali Kiba hapendi ndugu wa mumewe ambao wanaishi nyumbani kwa msanii huyo Tabata.

 “Siyo kweli vile ambavyo wamesema Amina hapendi watu, maisha yangu anayajua sababu nimeishi naye kwa miaka mitatu kabla ya ndoa, anapenda watu pia wasanii wangu wa Kings Music wana nyumba yao niliwanunulia maeneo ya karibu kabisa na kwangu Tabata. Wakija kwangu ni kunisalimia au kuja kurekodi.

“Vijana hawa ni kama watoto wangu, kuna muda nakaa nyumbani nawamisi na nawaita wanakuja nakaa nao, tunapiga stori na kutengeneza muziki lakini hawajahi kuingilia ‘privacy’ (faragha) yangu na mama Keyaan (mkewe) na kuna muda wanaweza wasionekane nyumbani kwa muda mrefu tu,” anasema Kiba.

NI KWELI AMMPA TALAKA MKEWE

Kiba anakiri kuwa na matatizo ya hapa na pale na mkewe japo kuwa hajaachana naye na hajampa talaka kama inavyosemwa katika mitandao ya kijamii.

“Ni kweli mimi na mke wangu tuna ugomvi wa hapa na pale ambao ni wakawaida kwa familia,” ANASEMA.

SABABU ZA KUMRUDISHA MKEWE KWAO

Kiba anasema: “Niliweza kumrudisha kwao mimi mwenyewe na sikumrudisha kwamba tumegombana ila nilikuwa na safari ya kwenda Uingereza kwenye ziara yangu.

“Nikampeleka kwao na nikaona kwanini nisimrudishe kazini aendelee kufanya kazi wakati mimi nipo huko, sababu alikuwa anaboreka na ananimbia anataka kufanya kazi sababu amesoma kichwa chake kitalala, nikaona ni vizuri kumrudisha kazini wakati sipo nyumbani mimi mwenyewe nilitaka, nilipotoka Uingereza nikamuuliza vipi unaendeleaje akasema yupo vizuri yeye na mtoto nikaona nimwache na kama kwenda kumwona nitakuwa nakwenda kila wakati.”.

TUHUMA ZA USHIRIKINA, KUPIGANA VIBAO

Kiba anasema:“Kuna mambo mengine yamefanya mpaka nijisikie vibaya, wanasema mambo ya ushirikina mara mama Keyaan anamroga mtoto wangu Sameer anaanguka. Hivi ni vitu vinavyostaajabisha na ishu ya kupigana vibao si za kweli.”

AUMIZWA NA MAMA YAKE KUHUSISHWA

Katika tetesi za Kiba kuachana na mkewe, mama mzazi wa msanii huyo alitajwa kama miongoni mwa chanzo cha kuvunjika kwa ndoa yake jambo ambalo siyo kweli.

 “Mama yangu ndiyo msuluhishi mkuu ikitokea mimi na mke wangu tuna ugomvi, sijapenda watu waliojaribu kumkosea adabu mama yangu, tuwaheshimu mama zetu, hata mke wangu ni mama,” anasema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles