22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Sababu tisa za mwanamume kutongoza

kutongozaNa Hamisa Maganga, Dar es Salaam

Wanaume huwa na sababu nyingi za kuwataka wanawake kimapenzi, lakini kubwa kuliko yote ni tama za kimwili, mengine huja baadaye.

Siku hizi mambo yamebadilika, hata wanawake huwa tunawatamani wanaume na kuwatokea.

Leo nitazungumzia sababu kadhaa za wanaume kuwatongoza wanawake. Sababu hizi zimetokana na utafiti nilioufanya kwa wanaume kadhaa wanaowatokea wanawake.

Anakujaribu

Mara nyingi wanaume wanapomtokea mwanamke huwa wanajaribu licha ya kwamba wakati mwingine hujikuta wakikubaliwa bila ya kutarajia. Wengi huwa wanatongoza kulingana na mazingira si kwamba amependa au ametamani, huwa wanajifurahisha lakini ukikubali hawakuachi.

 Tamaa

Tamaa ni sababu kubwa ya wanaume kutongoza. Uzuri, mvuto wa mwanamke husika huwa na nafasi kubwa kwa mwanamume kuvutiwa hadi akatongoza. Hii hutokana na ukweli kuwa kiasi kikubwa cha wanaume anapotongoza malengo yake inakuwa kukupata na kuweza kufanya mapenzi na mwanamke husika, masuala ya ndoa na kudumisha penzi huja baadaye.

 

Kupenda

Suala hili hutokea mara chache mno, kigezo cha kwanza cha mwanamume kutongoza huwa ni tamaa kupenda huja baadaye.

 

Kipoozeo

Wanaume wengine huwa na uhaba wa muda mrefu (kutu), hivyo anapokutana na msichana yeyote Yule hujikuta akimtokea ili mradi tu amalize haja zake baada ya hapo hakutafuti tena.

 

Hamaanishi

Kuna wanaume wengine huwa wanawatongoza wanawake si kwa lengo la kushiriki tendo la ndoa, bali anajaribu kucheza na hisia za mwanamke.  Wengine hufanya hivyo ili kuwaonyesha wanaume wenzao kuwa ana uwezo mkubwa wa kutongoza, kujionyesha kuwa yeye ni mwanamume asiyekataliwa na yeyote yule.

 

 Kukuoa

Mara nyingi mwanamume anayekufata kwa lengo la kuoa huwa ameshamchunguza mwanamke kwa kipindi kirefu, aidha kwa kuwatumia watu wa karibu na huyo binti au yeye mwenyewe kuchunguza nyendo zako bila ya kufahamu.

Ukiona mwanamume anakufuata na kutangaza kufunga ndoa nawe kwa kipindi kifupi, ujue umetimiza vigezo anavyotaka kwa mke wake, kama vile utulivu, upole, usafi, kufanya kazi na heshima kwa watu wanaokuzunguka. Lakini tambua kuwa hawezi kufunga ndoa na wewe kabla ya kushiriki tendo la ndoa, ni wanawake wachache mno wenye bahati hiyo.

 

Uhusiano 

Wanaume wengine wanapenda kuwa karibu na wanawake. Anapenda kuongozana na mwanamke hata kama hawashiriki tendo la ndoa, wakati mwingine anaweza kuwaambia marafiki zake kwamba ana uhusiano kimapenzi na fulani licha ya kwamba hajawahi kuuona mwili wake. Huwa anautunza huo uhusiano mpaka siku itakapotokea wamekutana kimwili, iwe kwa bahati mbaya au kwa kupenda.

 

Kukutumia

Wanaume wengine hupenda wanawake ambao wana uwezo kifedha. Kwamba hata ikitokea ana shida mwanamke awe tayari kumhudumia. Haoni tabu siku ya kwanza mmetoka akauchuna ili mwanamke alipe bili.

 

Kukuzalisha

Wanaume wa namna hii si wengi, lakini wapo. Wao lengo lao ni kupata mwanamke wa kuzaa naye na si kufunga ndoa au kudumisha penzi.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles