22.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

RT iweke mikakati thabiti Olimpiki

KWA kipindi kirefu sasa, mchezo wa riadha hapa nchini umeendelea kusuasua.

Umekuwa utamaduni wa kawaida kwa wanariadha wetu kurejea nchini mikono mitupu pale wanaposhiriki mashindano ya kimataifa.

Yapo mengi yamekuwa yakitajwa kuwa sababu ya mchezo huo kuwa kwenye hali mbaya, ikiwamo maandalizi duni ambayo hufanywa na wanariadha kabla ya kushiriki mashindano ya kimataifa.

Mara nyingi wanariadha wa Tanzania wamekuwa na maandalizi ya kulipua, yasiyoendana na ushindani uliopo kwenye mashindano ya kimataifa.

MTANZANIA pamoja na wadau wengi wa michezo kiu yetu ni kuliona Shirikisho la Riadha Tanzania(RT), likiufufua mchezo huo ambao miaka ya nyuma ulilitelea sifa na kuitangaza vyema taifa letu nje ya mipaka yake.

Hadi sasa ni wanariadha wawili tu, failuna Abdi na Alfonce Simbu waliofikia vigezo  vitakavyowawezesha kushiriki michuano ya Olimpili ambayo itafanyika Tokyo, Japan badae mwaka huu.

Tumekuwa tukisikia kaulu za matumaini kutoka kwa wanariadha na mamlaka zinazosimamia mchezo wa riadha, kwamba Watanzania watarajie medali.

Hata hivyo, ikiwa imebaki miezi michache kabla ya kuanza kwa michuano hiyo, hali ya mchezo wa riadha bado hairidhishi kiasi cha kuanza kuziota medali.

Hatukatai tunaweza kuambulia medali, lakini hofu yetu inaweza ikapatikana kwa kubahatisha na si kutokana na mipango thabiti ya RT.

Kwa tathmini ya haraka, inaweza kutuchukua hata zaidi ya miaka 10 na kuufanya mchezo wa riadha kufikia anga za majirani zetu Kenya, Ethiopia na Jamaica, si jambo la kipindi kifupi.

Bado changamoto za mchezo wa riadha ni nyingi mno na zinatakiwa kutolewa macho na si kuanza kuziweka akilini medali za Tokyo.

Kwa sasa, riadha si miongoni mwa michezo inayopewa nafasi kubwa katika shule zetu, mwamko ni mdogo katika ngazi za chini, pia viwanja vyenye ubora wa kimataifa ni tatizo sugu.

Kama changamoto hizo zitafanyiwa kazi, basi mchezo wa riadha hapa nchini utakuwa umepiga hatua kuliko kushinda medali Tokyo bila mipango thabiti.

Pia, kutokana na uwepo wa miundombinu inayosapoti maendeleo ya mchezo huo, kutakuwa na mwendelezo wa mafanikio ya wanamichezo wetu kwenye michuano ya kimataifa.

Kama Tanzania itafanikiwa kunyakua medali Tokyo ikiwa na kasoro hizo, hilo halitatufanya tuwe na imani ya kuvuna nyingine mwaka 2024.

Tutabaki kutegemea bahati na si mipango thabiti inayoweza kutumiwa na mwanariadha mwingine yeyote wa Tanzania kushinda medali.

RT kabla inatakiwa kupigania maandalizi ya wanariadha watakaoshiriki michuano hiyo na kuweka mikakati ya wale ambao hawajafikia vigezo waweze kufikia.

Watanzania wengi wana hamu ya kuona medali zinapatikana katika michuano hiyo mikubwa ya ngazi ya dunia na kuendeleza picha nzuri iliyoanza kutengenezwa ya wanamichezo na timu zetu za michezo tofauti ukiwemo soka kufanya vizuri katika medani ya kimataifa.

Tunafahamu mashindano hayo ni makubwa na yana ushindani, hivyo RT inatakiwa kutafuta namna ya| kuwasaidia wanaridha ili waweze kuvuna medali katika mashindano hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,415FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles