Meya Dar aondoa shauri alilofungua mahakamani

0
399

KULWA MZEE – DAR ES SALAAM

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita ameondoa shauri alilofungua mahakamani akidai alichokuwa akipinga ni kuondolewa, mchakato umefanyika lakini hauna madhara kwake.

Maombi ya kuondoa shauri hilo yaliwasilishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Janeth Mtega.

Wakili wa mleta maombi, Hekima Mwasipo aliwasilisha maombi hayo akidai kwamba wanaondoa shauri hilo mahakamani kwasababu walichukua wanaomba kizuiwe kufanyika kilishafanyika.

Anadai Januari 8, aliwasilisha maombi ambayo yalitolewa uamuzi Januari 10 wakati Januari 9, mchakato wa kumuondoa ulishafanyika.

“Tafsiri ya mleta maombi ni kwamba hayana maana, mteja wake hakupewa haki ya kusikilizwa, anaomba kesi iondolewe bila gharama, “amedai.

Upande wa wajibu maombi walikubali kesi iondolewe lakini waliomba iondolewe kwa gharama na mahakama ilikubali waleta maombi waondoe kesi kwa gharama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here