26.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Robertinho apangua kikosi

Na Mwandishi Wetu, Cairo

KUELEKEA mchezo wa marudiano wa African Football League dhidi ya Al Ahly, Kocha Mkuu wa Simba, Robertinho Oliveira atafanya mabadiliko ya wachezaji katika kikosi chake ili kupata ushindi katika mchezo huo.

“Nafahamu tutakuwa na mechi ngumu kesho dhidi ya timu kubwa Afrika ila kuna namna ambayo tutaingia na mpango wa tofauti na ilivyokuwa kwenye mchezo wa kwanza nyumbani. Nitakuwa na mabadiliko ya wachezaji kwenye baadhi ya maeneo ili kufanikiwa kucheza vizuri na kupata ushindi,” amesema kocha huyo.

Simba itaikabili Al Ahly Oktoba 24,2023 chini Misri baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Kutokana na matokeo hayo, Wanamsimbazi hao wanahitaji ushindi au sare ya kunzia mabao 3-3 ili kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles