27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Tyson wa Bongo achezea kichapo

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

BONDIA wa ngumi za kulipwa Hassan Ndonga maarufu Tyson wa Bongo, amegwa kwa pointi na Oscar Richard katika pambano la Safari ya Beach usiku wa Oktoba 22,2023.

Pambano hilo la raundi 10 limefanyika kwenye fukwe za Rongoni, Kigamboni jijini Dar es Salaam ambapo Oscar alipata ushindi wa pointi za majaji wote watatu.

Oscar ambaye ni bondia kutoka kambi ya Naccoz, amesema anatuma salamu kwa mabondia wote wanaotaka kuvunja utawala wa kambi hiyo kuwa anawakaribisha katika mpambano.

“Hassan ni bondia mzuri lakini mimi sio ‘level’ zake, ushindi huu unadhihirisha kuwa mimi ndiyo mkali wa derby na yoyote anayeka aje nipo tayari,” ametamba Oscar.

Kwa upande wa Ndonga amekiri kuzidiwa na mpinzani wake na kusema amebaini makosa atakwenda kuyafanyia kazi na yupo tayari kwa mechi ya marudiano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles